Wadau wa soka Afrika Mashariki leo wameshtukizwa na kifo cha gwiji wa soka nchini Kenya Mzee Joe Kadenge ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 akiwa hospitali ya Meridian jijini Nairobi alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wa marehemu , Oscar Kadenge amekaririwa akisema baba yake hakuwa vizuri kiafya kutokana na kupata shida ya kupumua pamoja na kupoteza uwezo wa kuona.
Wakati wa uhai wake akiwa mchezaji Kadenge alianza kucheza soka katika nafasi ya kiungo mshambuliaji na kisha mshambuliaji wa timu ya Maragoli United, kabla ya kujiunga na Abaluhya United (kwa sasa AFC Leopards) mwaka 1996.
Mwaka 2002 Kadenge aliifundisha timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na miaka miwili iliyopita Rais Kenyatta alimpa Kadenge shilingi milioni 2 za Kenya na kuamuru apewe kadi ya bima kwaajili ya matibabu.
Anakumbukwa zaidi kwa msemo wa ‘Kadenge na Mpira', uliotambulishwa na mtangazaji nguli wa wakati huo Leonard Mambo Mbotela.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments