''Tuache Mazoea'' - Mwasiti | ZamotoHabari.

''Tuache mazoea'' - Mwasiti
Dada mkuu kutoka kiwanda cha bongo fleva hapa nchini Mwasiti, amewachana wasanii wa kike kuacha mazoea na kufanya kazi.

Mwasiti amesema hayo kwenye mahojiano ya EATV&EARadio Digital, baada ya kuulizwa juu ya ugumu na ushirikiano kwa wasanii wa kike kufanya kazi pamoja.

"Mazoea tu, unajua watoto wa kike wengi huwa wanaangalia zaidi mazoea kuliko kazi. Mtu anaona kama mimi mwasiti, nitampigia simu Nandy ntafanya nae kazi, kwasababu mimi na Nandy tunaweza kuongea, tunaweza kucheka. Ili kazi ifanyike lazima kuwe na muunganiko kati yenu kwahiyo mara nyingi wanawake huwa tunafeli kutokana na mazoea na urafiki."

Mwasiti ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Serebuka remix, ambayo amewashirikisha mastaa wa kike kama N andy, Maua Sama, Chemical, Alice kyela na Stosh.

Na pia msanii huyo kashafanya kazi na wasanii wengi wa kiume kama Chid benz, Godzilla, Roma, Billnass, Ommy dimpoz, Ali kiba na wengine wengi.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini