Senegal wamefanikiwa kukata tiketi ya kutinga robo fainali ya Fainali za Michuano ya Afcon 2019 baada ya kuitungua Uganda bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.
Mapema tu katika dakika za awali, kulishuhudiwa mapambano makali, hali iliyosababisha mwamuzi kutoa kadi tatu za njano kutokana na mchezo usio wa kiungwana baina ya wachezaji. Nyota wa Senegal Sadio Mane aliwapa Senegal bao la uongozi mapema kabisa baada ya kupokea pasi kutoka kwa M’Baye Ning ambaye alitumia vizuri makosa ya mlinzi wa Uganda Godfrey Walusimbi aliyepoteza mpira kizembe.
Uganda walijitahidi kutaka kusawazisha bao mara kadhaa lakini juhudi zao ziligonga mwamba ikiwemo shuti kali la Emmanuel Okwi lililookolewa na mlinda lango wa Senegeal Alfred Gomis
Kipa na nahodha wa Uganda Dennis Onyango alizawadiwa kazi ya manjano baada ya kumchezea madhambi nje kidogo ya eneo la penati Sadio Mane dakika kumi tu baada ya mchezo kuanza.
Mane, ambaye kwa sasa ndiyo anyeongoza kwa magoli katika michuano hiyo akiwa na magoli 3 kibindoni alikosa mkwaju wa penati katika mchezo huo.
Hii ni mara ya pili anakosa penati katika michuano hii baada ya ile aliyokosa katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments