UJENZI WA MAHANDAKI RELI YA KISASA - SGR WAANZA RASMI MKOANI MOROGORO | ZamotoHabari.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Mhandisi Atashasta Nditiye azindua rasmi uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki ‘tunnels’ yatakayopitisha reli ya Kisasa – SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro  hivi karibuni .

Jumla ya Mahandaki 4 yenye jumla ya urefu wa Kilometa 2.6 yanatarajiwa kujengwa katika Mradi wa SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa ambapo handaki refu zaidi nchini linatarajiwa kujengwa likiwa na urefu wa Kilometa 1.031 sambamba na mahandaki mengine matatu ambayo yote kwa pamoja yataunganishwa na madaraja makubwa ili kuepusha athari za mafuriko ya mto mkondoa.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mbunge wa Kilosa, Menejimenti na Wafanyakazi wa TRC na Yapi Merkezi, wanahabari pamoja na wananchi wa wilaya ya Kikosa katika Milima ya Kilosa mkoani Morogoro. 

Waziri Nditiye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza menejimenti na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania kwa Usimamizi mzuri wa Miradi na kuwataka waendelee kuchapa kazi ili kuleta tija na mtokeo mazuri katika utoaji huduma bora za usafiri wa reli.

Aidha Naibu Waziri amewashukuru wananchi wa mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano wanaoonesha kwa wakandarasi na TRC, pia amewatoa hofu wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kuwa endapo serikali itahitaji eneo kwa ajili ya ujenzi, mwenye eneo atalipwa fidia pamoja na stahiki nyingine anazostahili kulipwa.

“Napenda niwahakikishie watanzania, kwa Yule amabaye tutamfuata kwenye eneo lake tutamlipa fidia yake” Amesema Mhe. Atashasta

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa ameongeza kuwa uthaminishaji wa ardhi ili kukabidhi maeneo yaliyobaki wa mkandarasi unaendelea na majedwali ya fidia yanafanyiwa kazi.
  Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano,Mh. Atashasta Nditiye akikata utepe jana julai 22,2019 kuashiria kuanza rasmi kazi ya uchorongaji  milima kwa mara ya kwanza Shirika la Reli Tanzania kwa ajili ya mahandaki ambayo watatumia kupitisha reli ya kisasa-SGR kwa kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa Morogoro- Makutupora katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri  Uchukuzi na Mawasiliano,Mh. Atashasta Nditiye akipewa maelezo baada ya kukata utepe jana julai 22,2019 kuashiria kuanza rasmi kazi ya uchorongaji  milima kwa mara ya kwanza Shirika la Reli Tanzania kwa ajili ya mahandaki ambayo watatumia kupitisha reli ya kisasa-SGR kwa kipande cha pili cha ujenzi wa reli ya kisasa Morogoro- Makutupora katika Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
 Muonekano rasmi uchorongaji Milima kwa ajili ya ujenzi wa mahandaki ‘tunnels’ yatakayopitisha reli ya Kisasa – SGR kipande cha Morogoro – Makutupora katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro 



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini