UVCCM Bahi waapa CCM kuibuka na ushindi uchaguzi wa Serikali za Mitaa | ZamotoHabari.

Na Charles James

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi [UVCCM] Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma umesema kuwa chama hicho kitashinda kwa kishindo kwa asilimia mia moja kwenye mitaa yote ya wilaya hiyo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bahi, Kadoke Hassan wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Wilayani humo.

Kadoke amebainisha misingi madhubuti itakayokipaisha chama hicho ni kutokana na Uongozi mzuri na Maridadi wa Rais Dk John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege, mradi wa bomba la kusafirishia Mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania pamoja na Mradi wa reli ya kisasa.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM amehamasisha vijana wote kushikamana na kujitokeza katika ushiriki wa serikali za mitaa na wasisite kuyatangaza Mazuri yanayofanywa na Rais Magufuli.

Aidha ,UVCCM wilaya ya Bahi umechukua fursa ya kumpongeza Mathias Lyamunda aliyekuwa Mgombea wa Ubunge mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi zake ndani ya Chama hicho na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli na Serikali ya CCM katika kuwaletea maendeleo Watanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bahi, Kadoke Hassaan akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa na namna walivyojipanga kuhakikisha wanashinda mitaa yote.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini