Wakulima wa Mahindi nchini wameshauriwa kutumia teknolojia rahisi na ya asili ya Vuta-Sukuma inayohusisha upandaji wa nyasi maalum na mimea jamii ya mikunde katikati na pembeni ya mazao ili kukabiliana na funza wa mabua ya nafaka na magugu hatari aina ya Kiduha ambayo yamekuwa yakifyonza madini na lishe iliyopo kwenye mimea na kuidumaza.
Hayo yameelezwa na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, kilichopo chini ya kitengo cha Afya ya Mimea, chini ya Wizara ya KIlimo,Chakula na Ushirika, Msami Elibariki, wakati akizungumza na wakulima wadogo wa wilaya ya Morogoro kwenye maonesho ya Kilimo ya wilaya hiyo.
Elibariki amesema Teknolojia hiyo ya Vuta-Sukuma inayotumia upandaji wa mimea jamii ya mikundekunde ijulikanayo kitaalamu kama Desmodium katikati ya mistari ya mahindi shambani, na nyasi aina ya mabingobingo (Black area ) ambayo huoteshwa pembeni kuzunguka shamba la mahindi na imekuwa ikisaidia pia kupatikana kwa malisho ya mifugo ambapo kama jamii yote mbili ya mimea ikitumiwa kwa kuchanganywa, husaidia ongezeko la upatikanaji wa maziwa toka kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Teknolojia hiyo ambayo kwa hapa nchini inatekelezwa na kituo cha kimataifa cha Physiolojia na Ikolojia ya wadudu (International Centre for Insects Physiology and Ecology -ICIPE) chenye makao yake makuu Nairobi nchini Kenya, imekuwa na Usimamizi wa kudhibiti wadudu waharibifu kwenye mazao ya Mahindi, Mpunga na Njegere kubwa (Chickpea), kwa nchi za Afrika Mashariki za Kenya,Ethiopia na Tanzania kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Misaada la Watu wa Marekani USAID.
Meneja Programu na Utawala kutoka ICIPE Nebiyu Solomon, wanaotekeleza mradi huo akasema umeanza kutekelezwa tangu mwaka 2016 kwa nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa kuanza na Morogoro, amesema kutokana na gharama kubwa ya mbegu hizo, wamewawezesha wakulima kuzipata bure kwa kuanzia ili waweze kuzipanda na kusambaziana, na akawahimiza wazalishaji wa mbegu kutumia fursa hiyo kuzalisha kwa wingi mbegu hizo ambazo zilizoletwa nchini zikitokea nchini Australia, ili kurahisisha upatikanaji wake.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, Msami Elibariki, akizungumza na wakulima wadogo wa wilaya ya Morogoro
Msami Elibariki, , Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, akizungumza na wakulima juu ya magonjwa ya mimea.
Teknolojia ya Vuta-Sukuma inayotumia upandaji wa mimea jamii ya mikundekunde ijulikanayo kitaalamu kama Desmodium katikati ya mistari ya mahindi shambani, na nyasi aina ya mabingobingo (Black area ) ambayo huote
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments