MENEJA Masoko na Mauzo kutoka Watumishi Housing ambao wanajishughlisha na uuzaji wa nyumba za bei nafuu Raphael Mwabuponde amewataka watumishi wote wa Serikali kununua nyumba kutoka shirika hilo la Watumishi Housing.
Amesema mtumishi wa serikali anapokosa nyumba ya kuishi ni aibu kubwa kwani kuna nyumba za bei nafuu kutoka shirika hilo.
Akizungumza katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea viwanja vya Saba saba jijini Dar es Salaam ,Meneja huyo amesema shirika hilo lina nyumba katika mikoa mingi hapa nchini, hivyo watumishi wanatakiwa kuchangamkia fursa hizo ili kuondokana na changamoto za upangaji.
"Kila mfanyakazi amepanga nyumba huku akisahau kuwa fedha hiyo anayolipa kwenye upangaji anao uwezo wa kupata nyumba kutoka Watumishi Housing kwani tuna mpango unaoitwa mpangaji mnunuzi na malipo yake utokana na kipato cha mtumishi huyo,"amesema Mwabuponde
Aidha ameongeza ili mtumishi wa umma uweze kuheshimika ni lazima uwe unamiliki nyumba.
Kwa upande Juma Ally ambaye ni mtumishi wa Serikali ameipongeza Watumishi Housing kwa jinsi inavyopambana kutoa misaada wa uelewa kwa watumishi katika umiliki wa nyumba Kwa watumishi wake.
Amesema kuwa jambo hilo ni njema kwani watumishi wanapomilikishwa nyumba kwa malipo ya bei nafuu na masharti ya kawaida, hivyo amewataka wananchi wengine kuchangamkia fursa hizo na si kutegemea pesa za kustaafu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Wakati huo huo Ofisa Uhusiano wa Watumishi Housing Meryjane Makawia amewataka pia wananchi wote kutembelea mahali pa miradi hiyo ilipo ili kujionea nyumba za kipee kutoka watumishi housing kwani ni za mfano na za kipekee na wala hazijawai kutokea hapa nchini.
"Siku zote katika maisha hakuna baba mwenye gari bali kuna baba mwenye nyumba hivyo ni bora watumishi wakakimbilia kununua nyumba na si magari,"amesema .
Aidha amewataka vijana na wananawake kujitokeza kwa wingi ili kujinyakulia nyumba za bei nafuu na zisizo na masharti.
Afisa Uhusiano na Masoko Watumishi Housing,Maryjane Makawia akizungumza leo jiji Dar as Salaam na Michuzi TV kuhusu wananchi wote kutembelea mahali pa miradi ya nyumba ilipo mikoa mbalimbali ili kujionea nyumba za kipee leo kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi Watumishi Housing Hellen Mwaihojo(kulia)kiwaelekeza wananchi namna kupata nyumba leo katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakiwa katika banda la Watumishi Housing katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba, jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments