Waziri Kabudi asema Mwandishi Azory Gwanda alitoweka na kufariki | ZamotoHabari.



Kutoweka kwa mwandishi mpekuzi nchini Tanzania Azory Gwanda hatimaye kumechukua sura mpya baada ya Waziri wa Mambo ya Nje nchini kusema kwamba mwandishi huyo 'alitoweka na kufariki'.

Katika mahojiano na BBC katika kipindi cha FOCUS ON AFRICA mjini London Waziri Palamagamba Kabudi alinukuliwa akisema kwamba visa vya watu kutoweka vimesababisha uchungu mwingi nchini humo.

''Wacha nikwambie unapozungumzia kuhusu kisa hicho, ni mojawapo ya visa ambavyo vimesababisha uchungu mwingi nchini Tanzania'' alisema.

Aliendelea kwa kusema,

"Katika eneo la Rufiji sio tu Azory Gwanda aliyetoweka na kufariki, nataka kukuhakikishia kwamba tunachukua kila hatua sio tu katika eneo la Rufiji bali pia maeneo mengine ya Tanzania ili kuhakikisha kuwa watu wetu wako salama-sio tu waandishi , bali pia Polisi na raia wa kawaida,".

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini