WIZARA YA ARDHI YAELEZEA NAMNA LESENI YA MAKAZI INAVYOPATIKANA | ZamotoHabari.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatumia Maonesho ya Biashara ya 43 ya Kimataifa yanayoendelea Dar es Salaam kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala yanayohusu ardhi na kubwa namna leseni za makazi .

Akizungumza na Michuzi TV kwenye maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Ofisa Ardhi wa Wizara hiyo David Malisa amefafanua leseni za makazi ni nyaraka inayotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa.

Amesema na sifa kubwa ya kutolewa leseni hiyo ni kwamba eneo hilo linatakiwa liwe limeendelezwa kiasi cha kuwa na msongamano mkubwa ambao hata uwekaji miundombinu muhimu kama barabara , mabwaya ya maji taka kutowezekana kuwekwa.

Malisa amesema pia leseni hiyo inaweza kutolewa katika maeneo ambayo Serikali ina mipango mingine baadae na kutoa mfano kuwa huenda kwa baadae Serikali inataka kufanya mradi mkubwa wa bandari au kujenga mradi mkubwa kama ule wa umeme wa mto Rufiji.

"Hivyo maeneo kama hayo wananchi wanaweza kupewa leseni ya makazi kwa kukaa nayo kwa mufa mfupi wakati wanasubiri kupisha mradi husika kulingana na uamuzi wa Serikali.

"Na kwamba leseni hiyo inatolewa kwa miaka mitano na ni nyaraka tu ya kumtambua mwananchi kwamba yeye ndio mwenye haki katika eneo hilo,"amesema.

Hata hivyo Malisa amesema katika maonesho hayo wananchi wengi wamekuwa na maswali lakini yanachanganya urasimishaji wa makazi ambao ni mpango mkubwa wa Wizara unaoendelea nchini na mpango wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi na kutoa leseni ya makazi.

"Nifafanua leseni ya makazi inatolewa katika eneo ambalo halijapangwa na wala halijapimwa na unaweza kushiriki kwenye mradi huo ambao unatekelezwa kwa Dar es Salaam wa kutambua na kusajili kila kipande cha ardhi lakini vile vile ukawa upo kwenye mpango wa urasimishaji,"amesema.

Ameogeza kuwa urasimishaji ni mchakato unaoendeshwa na kampuni binafsi kwa niaba ya Serikali na inafanya kazi kwenye mitaa ambayo inawezekana kupangwa kwa jinsi wananchi walivyoedeleza na kupimwa na kumiliki.Kampuni zinazofanya kazi hiyo zinatambuliwa na mamlaka husika.

Hata hivyo wananchi ambao wamefika kwenye banda la wizara hiyo kwa sehemu kubwa wamekuwa wakipata ufumbuzi wa changamoto ambazo zinawakabili katika ardhi.

Na wengine wamekuwa wapewa maelezo ya kufika kwenye ofisi za Serikali kwa ngazi zinazohusika na masuala ya ardhi ambako ndiko changamoto zao zinaweza kupata utatuzi sahihi.
 Ofisa Ardhi wa Wizara ya Ardhi,David Malisa akifafanua kwa Wananchi kuhusu leseni za makazi,kwenye banda lao ndani ya maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam,alisema kuwa Leseni za makazi ni nyaraka inayotolewa kwa mmiliki wa ardhi katika eneo ambalo halijapangwa wala kupimwa.Picha na Michuzi Jr.
 Mmoja wa Maofisa kutoka Wiara ya Ardhi akifafanua mambo mbalimbali kuhusu masuala ya Ardhi na kusikiliza baadhi ya Changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo wakati wa ufuatiliazi wa nyaraka zao za Ardhi,kwenye ya maonesho ya biashara ya 43 ya kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam 
 Pichani juu na chini baadhi ya Wananchi wakimsikiliza  Ofisa Ardhi wa Wizara ya Ardhi,David Malisa alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo Ardhi na mifumo mipya inayotumika katika kupata Ardhi na hatua zake. 



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini