Zari afunguka alivyokataa ndoa na Diamond Platinumz | ZamotoHabari.


Mwanadada tajiri raia wa Uganda na Mkazi wa Afrika Kusini mji wa Pretoria, Zarinah Hassan maarufu kama Zarithebosslady amesema alikataa kufunga ndoa na aliyewahi kuwa mpenzi wake na kumzalia watoto wawili, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz.

Zari amesema alikataa ombi hilo kufuatia sakata la Diamond kuzaa na mwanamitindo ambaye sasa ameingia kwenye sanaa ya muziki na anatamba na kibao chake cha ‘Boss’ alichomshirikisha Christian Bella, Hamissa Mobeto.

Ambapo kwa mujibu wa maelezo ya Zari anasema Diamond alitaka ndoa hiyo ifungwe ili kuzima maneno ya watu ambao waliingilia kati sakata lake la kuzaa na Hamisa na kutaka kuwagombanisha wawili hao.

Zari anasema Diamond alimdhalilisha sana kiasi cha kushindwa kumsamehe kwani yeye ni mtu mwenye jina kubwa Afrika Mashariki kitendo cha Nseeb kumdanganya kuhusu uhusiano wake na Hamissa hapo awali ni dharau kubwa sana na baadaye kufunguka kwenye vyombo vya habari alisikitishwa kwa kitendo hiko.


Zari hakuweza kukubaliana na Diamond suala la wawili hao kufunga ndoa kwani Diamond amekuwa mtu wa matukio hivyo ndoa hiyo haikuwa tiketi ya kumfanya  abadilika tabia yake ya kutembea na wadada mbalimbali, hivyo alimtaka Diamond kubadilika kwani anaamini kuwa ndoa ni tendo jema na la kuonesha upendo na si kuzima maneno ya watu kuhusiana na familia yake mpya aliyoitengeneza na Hamissa Mobeto.


Zari akihojiwa na Millard Ayo amesema’
”Nikamwambia Naseeb sio suala la mimi kuolewa na wewe ili kuzima skendo zako, bali ni suala la wewe kubadilika tabia yako, kwani kama tutaoana na tabia yako ikabaki vilevile tunakuwa hatujafanya kitu, naweza kuwa nahamu sana ya kufunga ndoa na wewe halafu ukawa na michepuko yako, ukazaa na wanawake wengine, hapana kwa sasa sihitaji kufunga ndoa na wewe”.amesema Zari.

Aidha, Zari ambaye ameachana na msanii huyo siku chache zilizopita amevalishwa pete na mtu wake mpya, na kusema kuwa hategemei kufanya sherehe kubwa kama ambavyo wengine wanafanya japo amekuwa na uoga mwingi sana kuingia katika ndoa kutokana kwamba tayari ana watoto watano.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini