BENKI YA NMB YAAHIDI KUENDELEA KUDHAMINI MASHINDANO YA GOFU | ZamotoHabari

 Pichani wa tatu kulia ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki



WACHEZAJI wa mchezo wa Gofu zaidi ya 100 wanatarajia kushiriki mashindano ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu huku Benki ya NMB ikiahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo kila mwaka.


Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo huwa ni maalum kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Majeshi ya Wananchi wa Tanzania ambayo hufanyika Septemba 1 ya kila mwaka huu lakini kutokana na ufinyu wa ratiba mashindano hayo yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8 ambayo itakuwa Jumamosi na Jumapili.

Akizungumza jana Agosti 22, 2019 jijini Dar es Saalam kuhusu mashindano hayo Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai amesema mashindano hayo hufahamika kwa jina la CDF NMB 2019 ambao ndio wadhamini wakuu."Siku ya Septemba 1 ya kila mwaka huwa ni Maadhimisho ya Siku ya Majeshi ya Wananchi Tanzania.Kutokana na ufinyu wa ratiba yatafanyika Septemba 7 na Septemba 8,"amesema.

Kapten Masai amesema wanatoa shukrani kwa Chama cha Gofu Tanzania kwa kukubali mashindano hayo yawe chini ya usimamizi wa Chama cha Gofu Tanzania na kuongeza zamani yalikuwa ni mashindano ya ndani lakini safari hii yatakuwa mashindano ya wazi.

Amesema mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa gofu kutoka wa ndani na nje ya Tanzania."Pia litajumuisha wachezaji wa kulipwa na wachezaji wa ridhaa.Kutakuwa na wachezaji chini ya miaka 18 na wachezaji kuanzia umri wa miaka 55 na kuendelea,"amesema Kapten Masai.

Ameongeza mwitikio wa mashindano haya ni mkubwa na kusisitiza wachezaji zaidi ya 100 wamethibitisha kushiriki kutoka vilabu mbalimbali vya nchini Tanzania.

"Tunatoa mwito kwa wachezaji wengine watambue mashindano hayo yatafanyika tarehe hiyo na hivyo muda bado upo wa kushiriki,"amesema Kapten Masai.
 
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi amesema huu ni mwaka wa nne sasa benki hiyo imekuwa ikidhamini mashindano hayo na wataendelea kudhamini mwaka hadi mwaka.

"Benki ya NMB imekuwa ikidhamini kwa zaidi ya miaka minne sasa na tukaona tuendelee kusapoti na tutaendelea kwani benki yetu ni wadau wakubwa wa majeshi yetu.


"Katika mashindano ya mwaka tumetoa Sh.milioni 21 kwa ajili ya kuyadhamini na hatujaishia hapo kwani kwa kutambua umuhimu wa michezo."Pia tumedhamini mashindano ya majeshi yanayoendelea Nairobi nchini Kenya kwa kutoa Sh.milioni 15 ambazo zimetumika kununua vifaa ya wachezaji wetu,"amesema.

Amefafanua hiyo yote inaonesha ushirikiano mkubwa kati ya NMB na majeshi ya Tanzania na wajisikia faraja kuendelea kushirikiana na majeshi yetu.

 Pichani wa pili kulia  ni  Ofisa Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB Filbert Mponzi  akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 21 kwa Nahodha wa Gofu kutoka Lugalo Kapten Japhet Masai,leo jijini Dar kwa ajili ya Udhamini wa mashindano ya Gofu yanayotarajiwa kufanyika Septemba 7 na Septemba 8 mwaka huu,ambapo zaidi wachezji 10o wanatarajiwa kushiriki


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini