BENKI ZA BIASHARA NCHINI ZASHAURIWA KUANZISHA HUDUMA YA UHIFADHI WA DHAMANA NA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI KATIKA MASOKO YA MITAJ, OFISA MTENDAJI MKUU CMSA ATOA PONGEZA BENKI YA I&M | ZamotoHabari.





Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama, akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji ya Benki ya I&M  jijini Dar es Salaam Agosti 26.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M  Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M , Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

Mkuu wa Idara ya Wateja wa RejaReja Benki ya I&M  Lilian Mtali.

Meza Kuu.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&MBank , Baseer Mohammed, akizungumza katika uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji.

Baadhi ya wageni waalikwa.

Meneja Msaidizi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji Benki ya I&M , Frank Bunuma, akizungumza kuhusu Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji iliyozinduliwa na benki hiyo.



OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama ametoa mwito kwa benki za biashara kuanzisha huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji kwani hatua hiyo ni muhimu na itazisaidia benki hizo kuongeza idadi ya wawekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Aidha amezishauri benki zote hapa nchini kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ikiwemo kuuza dhamana kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam ili kuongeza mitaji yao.

Mkama amesema hayo leo Agosti 26 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji wa Benki ya I&M ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza hiyo ni uthibitisho sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Amesema hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa agizo la Serikali kwa benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha ili kuweza kujiendesha kibiashara. Aidha,ametoa mwito kwa kampuni za bima kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ili kuongeza mitaji yao.

Amesisitiza hiyo itaziwezesha kampuni za bima hapa nchini kuwa na uwezo wa kushindana na kampuni za nje zinazotoa huduma ya bima (underwriting risks) hapa nchini. Vile vile, natoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na taasisi za fedha kuunga mkono malengo na azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda kupitia masoko ya mitaji nchini.

Akizungumzia Benki ya I&M,Mkama amesema kuwa benki hiyo amesema imefanikiwa kupata leseni kutoka kwa Mamlaka hiyo ya kutoa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji kwa mujibu wa kanuni za masoko ya mitaji na dhamana za mwaka 2006.

Amesema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo ya masoko ya mitaji nchini, kwani benki ya I&M inakuwa ni benki ya saba kati ya benki za bishara 40 zinazofanya shughuli zake hapa nchini, kupata idhini ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji na dhamana hapa nchini.

Ametumia nafasi hiyo kutumia fursa hiyo kuipongeza bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Benki ya I&M pamoja na taasisi na wadau wote waliohusika katika kufanikisha hatua hiyo muhimu na kwamba masoko ya mitaji ni sehemu muhimu katika sekta ya fedha nchini. Sekta hii inasaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

Amefafanua masoko ya mitaji hujumuisha uuzaji wa hisa za kampuni (shares), hatifungani za kampuni (Corporate Bonds), hatifungani za Serikali Kuu (Government Bonds), hatifungani za Serikali za Mitaa (Municipal Bonds), na vipande katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).

Mkama amesema hivyo masoko ya mitaji husaidia pia kurekebisha kiwango cha ukwasi na mfumuko wa bei katika uchumi. Aidha, sheria na taratibu za masoko ya mitaji zinazitaka kampuni zilizopo katika masoko ya mitaji kujiendesha kwa uwazi wa hali ya juu na kwa kufuata kanuni za utawala bora. Matokeo ya masharti haya ni kwamba mara nyingi kampuni hizo hufanya kazi kwa ufanisi na kwa kuwa taarifa zao za fedha ziko wazi ni rahisi kwa serikali kukusanya kodi stahiki.

Amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji ni huduma inayotolewa na benki za biashara na ili kutoa huduma hii ni lazima kupata leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na kwamba wanaopata leseni hiyo hutoa huduma hiyo kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Pia amesema Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji hutoa huduma za utunzaji wa dhamana: akaunti za dhamana za wawekezaji huifadhiwa na kusimamiwa kwa umakini na benki za biashara (custodians) ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa za siku kwa siku kuhusu thamani halisi ya dhamana hizo.

Mkama ametaja nyingine ni utunzaji wa mapato ambapoo wawekezaji hupatiwa taarifa kuhusu faida za uwekezaji wao ikiwa ni pamoja na kuwekewa gawio au riba kwenye akaunti zao pale uwekezaji wao unapokuwa umepata faida. Ukamilishaji wa miamala ya dhamana kwa kuhakikisha miamala ya dhamana inakamilika vizuri, kwa uhakika na kwa wakati kulingana na maelekezo ya mwekezaji na matakwa ya sharia, kanuni na taratibu zote.

Pia Utoaji wa taarifa kwa maana ya kutengeneza taarifa mbalimbali kuhusu uwekezaji husika kama vile muhtasari, salio la akaunti na taarifa za siku. Pia kutengeneza taarifa atakazohitaji mwekezaji kuhusu uwekezaji wake na utunzaji wa fedha ili kuwezesha uwekezaji zaidi, utunzaji wa fedha ni muhimu. Utunzaji wa fedha unahusisha kuwa na taarifa moja ya fedha kutokana na vyanzo vyote vya mwekezaji, kusaidia uamuzi wa uwekezaji na dhamana husika, kufanya uwekezaji, kuratibu fedha kutokana na uwekezaji na kuratibu mtiririko wa fedha

“Kwa huduma hii wawekezaji huwakilishwa katika mikutano mikuu ya mwaka ya kampuni walizowekeza dhamana zao, na hivyo kupata fursa ya kushiriki katika maamuzi yote ya kampuni hizo. Kwa ujumla, huduma hii ni muhimu kwani inarahisisha uwekezaji katika masoko ya mitaji na hivyo kuchangia kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira.

“Aidha huduma hii inachangia kuongezeka kwa idadi ya wawekezaji wa kigeni na hivyo kuchangia kuongezeka kwa akiba hapa nchini; kuongezeka kwa mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali; na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa, ninyi mliohudhuria hafla hii, na hasa waandishi wa habari mtaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji”,

Amesema kuwa kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Viwanda, mahitaji ya fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo hususani miundombinu yanaongezeka. Serikali na kampuni binafsi zinaweza kujipatia fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa njia ya kuuza hisa, hatifungani na bidhaa zingine za masoko ya mitaji. Ili kufanikisha azma hiyo kunahitajika kuwepo kwa benki nyingi za biashara zinazotoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji.

Amoengeza hatua hiyo ni muhimu kwani inachangia kuongezeka kwa uwekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Viwanda hapa nchini. Hivyo anao ujasiri wa kueleza benki ya I&M imekuja katika wakati muafaka. Pia leseni hiyo ya benki ya I&M kwa ajili ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ni mojawapo wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Benki I&M Hongereni Sana.

Pia amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji inawezesha na kurahisisha biashara kwa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa. Itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha 2014/1015, Kanuni za Masoko ya Mitaji na Dhamana (Wawekezaji wa Kigeni) za 2003 zilirekebishwa ili kuruhusu ushiriki wa bila kikomo wa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa.

Hivyo watoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ndio wanaoweza kuingia mikataba na wageni kwa ajili ya kutoa huduma hiyo. Kwa sababu hiyo, inatarajiwa kuwa kuongezeka kwa huduma hiyo kutaongeza biashara katika soko la hisa inayohusisha wawekezaji wa nje ya nchi.

Pia amesema benki ya I&M ina uhusiano mzuri na benki washirika katika nchi mbalimbali kama vile Kenya ambao wanatoa huduma kama hii. Pia inao uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika masoko ya mitaji na hivyo kutawezesha wawekezaji wa Afrika ya Mashariki na kwingineko kuweza kuingia Tanzania kirahisi.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini