Darassa Afunguka Ishu za kuumizwa Katika Maisha | ZamotoHabari.

Msanii Darassa 'CMG' au "Mr Burudani" kama anavyojiita, amefunguka kuhusu 'issue' za kuumizwa katika maisha yake na kumnunulia gari 'Producer' Abbah.


Darassa amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital baada ya kuulizwa kama alishawahi kuumizwa katika maisha yake ambapo amesema,

"Mimi kuniumiza lazima ufanye kazi ya ziada, huwa naishi katika sababu za maisha ambazo zinatoa changamoto, furaha, wakati mzuri na mbaya, nyakati za kushuka na kupanda, kuwaza, kiza, mwanga kila kitu. Ukishazijua sababu za maisha na ukishajua kama kuna Mungu, mtu kama huyo kumshusha lazima ufanye kazi ya ziada sana".

Aidha msanii huyo amezungumzia suala la kumnunulia gari la siri mtayarishaji wa muziki 'Producer Abbah' na kusema Abbah ni mtu ambaye yupo kwenye familia yake na ameamua kutotangaza kwa sababu amefanya kwa mtu anayempenda.

Pia amesema amempa gari hilo ni kama zawadi kwa kile anachomfanyia na sio kama makubaliano ya kazi kama akifanya vizuri iwe lazima kumnunulia gari.




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini