Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima amemtaka dereva wake asifikirie hasara ya gari iliyopatikana na badala yake kumfikiria kumpoteza mtoto wake Kasobi Shida (26), kwani yupo tayari kupanda hata bajaji wakati akisubiria kupatiwa gari jingine.
Malima amewaongoza mamia ya wakazi wa Musoma sambamba na watumishi wa serikali na taasisi za umma na binafsi katika mazishi ya kijana huyo aliyefarikia usiku wa kuamka Jumatano kutokana na ajali aliyoipata mkoani Mara.
Kasobi alifariki kutokana na majeraha ya tumbo aliyopata katika ajali aliyoipata baada kuchukua gari ambalo baba yake hutumia kumwendesha Mkuu wa Mkoa, Adam Malima, Agosti 4 mjini Musoma.
Kijana alichukua gari hilo bila ruhusa ya baba yake akiwa kwenye mwendokasi lilimshinda na kulipigisha katika mtaro.
Malima akitoa salamu za pole amemtaka dereva huyo kutokufikiria thamani ya gari hilo ambalo limeharibika kabisa badala yake amfikirie marehemu mtoto wake.
Amesema kuwa hakuna haja ya dereva wake huyo kufikiria kuhusu gari hilo na kwamba tayari serikali imeanza utaratibu wa kumpatia gari huku akisema kuwa yuko tayari kutumia hata bajaji wakati utaratibu ukifanyika ili apewe gari lingine.
“Ndugu yangu amefiwa na mtoto wake ambaye kwangu ni mtoto wangu nimekuja kumzikia ndugu yangu mtoto wake hayo mengine hayana nafasi kwa sasa. Gari limekwisha teketea hatuna namna kikubwa tumuombee kijana wetu apumzike kwa amani,” alisema Malima.
Aliongezea kuwa:”Juzi nilikwenda kuwaona wote hospitali nilianza na Shida nikaona kuna hali za huzuni wengine wanasema Kasobi kafanya nini..alichokifanya Kasobi huenda katunusuru sisi,” alisema
Malima ameitaka jamii kuungana na familia ya dereva wake katika kuomboleza na kuwafariji badala ya kuhangaika na maneno ambayo yanasemwa na kuandikwa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio hilo.
Alisema kuwa mambo mengi yanayosemwa hayana ukweli na kwamba huu sio muda muafaka kwa ajili ya kujibu mambo hayo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments