Huawei Yaendelea Kufanya Vizuri Sokoni Licha ya Vitisho Kutoka Marekani | ZamotoHabari.

Huawei Yaendelea Kufanya Vizuri Sokoni Licha ya Vitisho Kutoka Marekani
Kampuni ya Huawei imesalia kuwa muuzaji namba mbili wa simu kote duniani katika robo ya pili ya mwaka 2019 licha ya vitisho vya vikwazo kutoka Marekani.

Shirika la Strategy Analytics kwenye tathmini yake limesema Huawei imefanikiwa kuongeza mauzo yake licha ya kuwa na mdororo wa soko la simu kote duniani.

Kulingana na Strategy Analytics, mauzo ya simu kote duniani yalipungua kwa asilimia 2.6 huku simu milioni 341 zikiuzwa kati ya Aprili na Juni mwaka huu.

Samsung ya Korea Kusini ambayo inaongoza kwa mauzo ilikuwa na ongezeko la asilimia 22 huku nayo Huawei ikiwa na mauzo ya asilimia 17 nayo Apple ya Marekani ikiwa na asilimia 11.

Na kulingana na tathimni ya shirika la Counterpoint, kwa jumla mauzo ya simu kutoka China kwa kampuni Huawei, Oppo, Vivo, Xiaomi, na Realme yalifikia asilimia 42.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini