Liverpool 3 Arsenal 1: Dondoo Muhimu za Mchezo huo | ZamotoHabari.


Liverpool jana usiku wameibamiza Arsenal mabao 3-1 katika Mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika kwenye Uwanja wa Anfield na kuendeleza ubabe dhidi ya Washika Mitutu hao.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Joel Matip dakika ya 41 na Mohammed Salah dakika 49 na 58 kwa njia ya penati.

Goli la kufutia machozi la Arsenal limefungwa na Lucas Sebastián Torreira Di Pascua dakika ya 85.

Dondoo muhimu za kufahamu
Tangu Jurgen Klopp akabidhiwe mikoba ya kuinoa Liverpool Oktoba 2015, Liverpool imefunga magoli 26 katika michezo nane ya Ligi ya England dhidi ya Arsenal-Idadi kubwa zaidi ya magoli kwa timu moja kuifunga timu nyingine kwa kipindi hicho.

Ni Everton pekee ambao wamruhusu magoli mengi zaidi ugenini kwa mpinzani mmoja (Liverpool) katika Ligi Kuu England kuliko Arsenal. Everton wamefungwa magoli 64, Arsenal magoli 62.
Kwa sasa Arsenal wameshindwa kushinda mechi zozote zilizopita 23 za ugenini dhidi ya ‘Big Six’ (Sare 8, Kufungwa 15)

Tangu kuanza kwa msimu uliopita, Arsenal wamesababisha penati 8. Ni Brighton tu wamewazidi Arsenal kwa kusababisha penati 10.

Liverpool wamefunga magoli 22 ya kichwa katika Ligi Kuu England tangu kuanza kwa msimu uliopita. Magoli saba zaidi kuliko timu nyingine yoyote. Tayari wameshafunga magoli matatu kwa kichwa msimu huu wakati huo huo hakuna hata timu moja iliyofunga zaidi ya goli moja kwa kichwa.
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amecheza mechi nane na Arsenal kwenye Ligi Ya England bila kufungwa (Kushinda 5, Sare 3).

Mohamed Salah amehusuika moja kwa moja kwenye magoli dhidi ya Arsenal kwenye Ligi Kuu England kuliko timu nyingine yoyote (Mechi nane; Magoli sita, pasi za magoli mbili). Amefunga kwenye mechi zote nne za nyumbani dhidi ya Arsenal.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini