MIKONONI MWA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MITATU | ZamotoHabari.


Na Mwamvua Mwinyi,Pwani 

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Dismas Silyvester (35) kwa tuhuma za  kumbaka mtoto mdogo mwenye miaka mitatu(jina limehifadhiwa), huko Mlandizi A ,kata ya Mlandizi ,Kibaha .

Akithibitisha kutokea kwa tukio la kwanza ,Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wankyo Nyigesa amewaambia waandishi wa habari kwamba, Dismas anatuhumiwa pia kumuiba mtoto wa miaka mitatu na kwenda nae kichakani na kumfanyia unyama huo. 

"Baada ya taarifa kutolewa kwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema lilimkamata mtuhumiwa na mtoto mchanga huyo katika mashamba ya mbogamboga vichakani,"amefafanua Wankyo.


Wankyo alieleza ,uchunguzi unaonyesha mtoto huyo ambae jina limehifadhiwa ,ameingiliwa kimwili.

Katika tukio jingine,Kamanda Wankyo amesema Agosti 25, mwaka huu, saa saba mchana katika eneo la Msongola, Mariam Shomari aligundua kuibiwa mtoto wake mchanga Swaumu Sudi mwenye miezi mitatu.

"Mtoto huyo aliibiwa ndani akiwa chumbani alipokuwa amelala baada ya mama yake kutoka kwenda kuomba kibiriti kwa jirani umbali wa mita 200 na mwanamke ambae hajafahamika hadi sasa,"amesema.


Inadaiwa mwizi huyo wa mtoto alitumia mbinu ya kuvizia mama wa mtoto kutoka na yeye kufika kwenye nyumba hiyo na kumwambia mtoto mdogo Fatima Sudi miaka mitatu aliyekuwa amebaki na mdogo wake kuwa ametumwa na mama yake kuja kumchukua mtoto huyo ili ampelekee na kufanikisha wizi huo.


Amesema jeshi la Polisi mkoani hapa linaendesha msako mkali wa kumtafuta mwizi wa mtoto ambapo ametoa mwito kwa viongozi wa Serikali za mitaa ,watendaji wa kata ,wenyeviti wa vitongoji na vijiji pamoja na jamii kutoa taarifa iwao watamtilia shaka mtu ambae anaonekana na mtoto asiye wake.





Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini