Mwanamke Akipewa Uhuru Sana Heshima yake inashuka | ZamotoHabari.


Wanawake wanapenda uhuru sana lakini hawajui athari za uhuru. Tumeshuhudia katika zama hizi za Utandawazi wakidai haki mbalimbali ikiwemo haki ya maamuzi katika mitindo yao ya maisha mathalan mitindo ya mavazi.

Bila ya wao kujua mchawi ni nani. Wamejikuta wakilalamika na kuona kadiri siku ziendavyo ndivyo heshima yao inashuka. Mchawi ni wao wenyewe.

Ile heshima waliyokuwa wakipewa zamani sasa imepungua kama sio kuisha kabisa. Kwa sasa thamani ya wanawake imepungua si ajabu inaweza kuthaminiwa na pesa na kununulika kama bidhaa tuu.

Siku hizi ukihitaji mwanamke huna haja ya kufikiri wala kuumiza kichwa sana kutokana na kuwa 80% ya wanawake hununulika tena kwa kipande cha mkate tu. Ni jambo linalosikitisha sana. Tena lenye kuumiza zaidi na zaidi na kupoteza ule utukufu wa mwanamke.

Kuachiwa uhuru uliopitiliza kwa wanawake kumepelekea vijana kukosa hamasa ya kuoa. Iweje waoe ikiwa huduma zote wanazipata. Si rahisi kuoa mwanamke bikra katika zama hizi. Na hii pia inaweza kuelezea uhuru uliopitiliza kwa wanawake. Ingawa jambo hili linachangiwa na sababu nyingi lakini sababu kubwa ni uhuru uliopitiliza.

Ili familia iwe imara mbali na Kuwa na Upendo lakini mwanaume lazima alinde Uhuru wa Mke wake. Asimpe uhuru kupitiliza. Uhuru wa kuongea na kila mtu. Uhuru wa kuvaa atakavyo na kuonyesha maumbile yake. Uhuru wa matembezi atakavyo. Uhuru wa kurudi nyumbani. Uhuru wa kusema hovyo hovyo hasa matusi. Hata anguko la Eva pale Eden ni matokeo ya Adam kumpa Eva uhuru wa matembezi uliopitiliza na matokeo yake akakutana na Mlaghai.

Ona sasa Wanawake wanavyodhalilika. Ona jinsi wanavyonyanyasika licha ya kuwa wao ni viumbe muhimu katika huu Ulimwengu. Kila ukipita ni matusi kuwahusu. Kila ukipita unasikia lugha chafu ya viungo nyeti vya hawa Wanawake zetu. Kila ukipita unaona picha mbaya zinazowadhalilisha kina mama. Huko kwenye Media, Muziki na Filamu hakufai. Wanawake wanadhalilika.

Yote hii ni kuwapa uhur uliopitiliza katika mitindo ya mavazi. 90% ya wanawake duniani hawajielewi. Wao hufikiri kuvaa mavazi ya uchi ni dalili ya ufahari na matambo ya kuvutia wanaume. Hilo ni kweli kabisa wanaume tuliokamalika tunatamani lakini si katika viwango vya kukuheshimu na kutamani kukuoa. Tunatamani katika zinaa na uasherati. Sio lazima umvutie mwanaume kwa kujidhalilisha. Zipo njia nyingi za kumvutia mwanaume na kumfanya akuheshimu kulingana na lengo lako. Kama lengo lilikuwa akutongoze ili uwe mke wake zipo njia nyingi tuu.

10% ya wanawake duniani ndio wanaojielewa. Hawa hujua thamani yao. Hujua kuwa uhuru unamipaka yake. Na hata wakikutana na Mwanaume asiyejielewa ambaye anashindwa kuilea familia kwa kukemea tabia mbaya. Mwanamke huyo atabeba jukumu la kumfunza bintiye adabu, Miiko na mipaka ya uhuru wa mtoto wa kike.

Raha ya mwanamke ni kujisitiri. Heshima yake ipo kama atajua umuhimu wa maumbile yake. Ndio maana Aliyeumba mbingu na nchi akatoa maagizo ya wao kujisitiri. Kukiuka agizo hili ni kujidhalilisha. Kama tunavyoona siku hizi.

Kuwapa wanawake uhuru uliopitiliza ni kuuharibu ulimwengu. Ni kuhamasisha uzinzi na uasherati. Wazee wa zamani sio wajinga kusema wanawake ikifika jioni wawe nyumbani. Wanawake wakitoka dukani wawe na mtu wa kuwasindikiza. Wanawake wasidhurure hovyo. Wasiwe na urafiki na wanaume wasio ndugu zao. Watunze bikra zao ikiwa ni alama ya uaminifu na usafi.

Kukiuka haya na kuwa uhuru tunaona matokeo yake sasa kama vile Wanatembea wakiwa uchi kabisa, Uzinzi umeongezeka mara dufu, Wanawake wanaozalia nyumbani bila ndoa wanaongezeka hii hupelekea mtoto kulelewa na upande mmoja. Wanawake kutoridhika na maumbile ya waume zao kutokana na kutojitunza vizuri wakati wa usichana. Wanawake kuchepuka hovyo hovyo kwa kushindwa kuwa waaminifu miongoni mwa athari zingine.

Kama dunia inahitaji maadili safi basi ni lazima Uhuru wa mwanamke ujadiliwe na kuangaliwa upya. Udhibitiwe kwa maslahi ya maadili na kutunza heshima yao. Najua haitawezekana kwani kupitia uhuru wa wanawake makampuni ya kizungu na ya magharibi hujipatia fedha nyingi kwenye urembo na mavazi. Pia ni kama agenda ya kuendelea kuzifanya nchi za Afrika ziwe na migogoro ya kifamilia ambayo ndio chanzo kingine kikubwa cha Umasikini. Kama wanawake wakiharibika basi ni wazi jamii husika imeharibika.

Kudhibiti uhuru wa mwanamke ni kulinda heshima ya mwanamke. Lakini kadiri wanavyopata uhuru ndivyo heshima yao inavyopotea.

Wito wangu; Kila mwanamke ajitathmini na kuomba muongozo kwa baba zao. Na kama Baba alikimbia au alifariki kuomba Muongozo kwa Wajomba au Baba wakubwa na wadogo au Viongozi wa dini. Au Muongozo kwa waume zao.

Andiko hili nimeliandika kwa lengo la kutambua na Kulinda heshima ya mwanamke kwa kudhibiti uhuru uliopitiliza ambao binafsi naona ndio chanzo kikuu cha kudhalilika kwa wanawake. Andiko hili lisihusishwe na wale wanaowanyanyasa wanawake kwa kutowapa haki za msingi kama vile elimu, Afya, Urithi wa mali, Kufanya kazi n.k.

Imeandikwa na;
Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.
0693322300
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini