Baadhi ya wananchi wakiwa wanatoka eneo lenye mgogoro ambapo walitaka eneo hilo la mto waweze kilitumia kwa ajili ya kulishia mifugo pamoja na kulima katika mto huo ambapo kutokana na hali hiyo mto huo usingeweza kudumu kwa muda mrefu
Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha ( kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati walipotembelea eneo amvalo lilikuwa na mgogoro kati ya Kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous
Aniel Heliem mmoia wa wananchi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Cinstantine Kanyasu mata baada ya kuutangaza kuwa eneo la Kihurumila si sehemu ya Pori la Akiba la Selous na wala sio eneo la Kijiji cha Kikulyungu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akionesha eneo la Pori Tengefu akiwa kwenye kigingi ambacho ni mpaka kati ya eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka wakiwa kwenye eneo la kigingi huku Mbunge huyo akiomuonesha Naibu Waziri Kanyasu eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Baadhi ya wananchi wakiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakiangalia eneo la Kihurumila sehemu ambayo kuna mto na ambalo lilikuwa na mgogoro kuwa sio mali ya pande zote mbili bali mali ya serikali kuu inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mbunge wa Liwale, Mhe.Zuberi Kuchauka akizungumza na wananchi wake kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 12 baada ya Naibu Waziri Kanyasu kuzungumza na wananchi hao
…………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 12 baina ya Pori la Akiba la Selous na Wananchi wa kijiji cha Kikulyungu kilichopo katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Mgogoro huo wa ardhi ulianza mwaka 2007 ambapo wananchi walianza kudai kuwa eneo la Kihulumira ambalo linapakana na Pori la Akiba la Selous kuwa ni moja ya maeneo yao ya Asili.
Kufuatia hali ilipelekea uhasama mara kwa mara kati ya wananchi na askari wanyamapori hasa pale wananchi walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa wameingia ndani ya Hifadhi bila kibali.
Akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo lililokuwa na mgogoro, Kanyasu alisema eneo hilo lilisajiriwa mwaka 1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka 2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya kijiji.
Amesema baada ya kuundwa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazo ilibainika kuwa eneo hilo si la wananchi na wala sio sehemu ya Pori la Akiba la Selous bali ni Pori Tengefu ambalo ni mali ya serikali Kuu na linasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katika hatua nyingine, Kanyasu amewataka wananchi kuacha vitendo vya kukata miti ovyo na kuchoma misitu kutoka na uharibifu mkubwa wa misitu aliuona karibu na eneo lililokuwa na mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo kuweka sheria kali ili kudhibiti hali ya uharibifu wa misitu unaoendelea katika maeneo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachi wa wilaya ya Liwale Mbunge Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa haujapatiwa ufumbuzi
Amesema mgogoro huo uliwafanya wananchi wa maeneo hayo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo badala yake wajanja wachache walikuwa wakitumia nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.
” Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi” Alisisitiza Kuchauka.
Kutokana na kumalizika kwa mgogoro huo wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kulitumia eneo hilo kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ili kuinua kipato katika kijiji hicho
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments