NEWZ ALERT: WATU WENGI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA MSAMVU,MOROGORO BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA MOTO. | ZamotoHabari.

Ínaripotiwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kuungua moto na kupoteza maisha baada ya tenka la mafuta kuwaka moto eneo Msamvu Itigi mkoani Morogoro asubuhi hii. 

Inadaiwa kuwa chanzo  ni watu kutaka kuiba betri kutoka kwenye tenka hio iliyokuwa imepinduka huku wengine wakiiba mafuta, ndipo moto ukalipuka. Juhudi za kuopoa miili zinaendelea.

Aidha Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa lori la mafuta (petroli) lilipinduka, hivyo watu mbalimbali, wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki wakaenda eneo la tukio na vibebeo kwa lengo la kupata mafuta. 

Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimekwishawasili eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa kadiri itakavyowezekana,ikiwemo na kubaini idadi ya watu waliopoteza maisha.  

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

TUNAENDELEA KUSUBIRI TAARIFA RASMI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA.






Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini