Polisi Aliyempiga Risasi SABA Mpenzi Wake Baada ya Kumsomesha Chuo na Kuja Kumkataa Alipomaliza | ZamotoHabari.


Patrick Oita Nyapara, ambaye ni police nchini Kenya alimuua mpenzi wake kwa kumtandika Risasi 7 baada ya binti huyo kumkataa, pindi alipomaliza masomo Chuo Kikuu.
Kwa maelezo ya Patrick ni kwamba alimchukua mdada huyo aliyejulikana kwa jina la Christine Maonga kutoka katika familia duni kijijini na kumpeleka mjini Nairobi kama mke wake ambapo aliamua kumsomesha mpaka chuo kikuu.

Alikuwa akimlipia karo na mahitaji mengine pamoja na kutuma pesa kwa mama mzazi wa binti huyo kama msaada kutokana na familia hiyo kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha.

Baada ya kuhitimu masomo yake, Christine alimwambia Patrick kuwa amechoka kuwa naye kwani ni mtu asiyekuwa na hadhi yoyote na hafai kuwa mpenzi wake hivyo ni vyema kila mtu afanye mambo yake.

"Nimepata mpenzi mwingine ambaye ananifaa sana pia ni Mkurugenzi wa Kampuni moja kubwa sana jijini Nairobi hivyo siwezi kuwa na wewe Patrick mtu usiyekuwa na future na ni daraja D ambalo ni dhaifu kwangu", alisema Christine.

Patrick hakuielewa kauli ya mpenzi wake, akaamua kwenda kijijini kwa mama yake na Christine kuomba msaada wa suluhu ili aweze kumuoa binti yao kwani alikuwa ametumia gharama kubwa mno kumsomesha.

Mama yake binti alijibu kuwa hawezi kumpangia mtoto wake mume wa kumuoa hivyo anapaswa aachwe ajiamulie yeye mwenyewe. Patrick hakukubali, akamtafuta dada yake Christine na kumwelezea hali halisi lakini alijibiwa kuwa hana hadhi ya kumiliki mwanamke aliyehitimu Chuo Kikuu hivyo atafute mwanamke wa level ya mgambo kama yeye.

Aliondoka na kurudi nyumbani na kuchukua uamuzi mgumu wa kumuita Christine nyumbani kwa lengo la kuongea na kumaliza tofauti zao ili waachane kabisa, binti alienda nyumbani kwa Patrick mapema zaidi. Alifika na kumkuta Patrick amejihami kwa silaha, hawakuzungumza chochote zaidi ya kumkandamiza risasi 47 na zote zikapita mwilini mwa Christine hali iliyopelekea kifo chake papo hapo.

Nini maoni yako?
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini