MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii ya Mystyle, natumai unaendelea poa na shughuli za kulijenga taifa. Kama unaumwa, basi Mungu akupe nguvu na upone haraka, urudi kama kawaida.
Jumamosi ya leo tunamleta kwenu msanii wa muziki na filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ambaye anaelezea maisha yake kuanzia siku inaanza hadi inamalizika, ungana naye hapa chini;
My Style: Mashabiki wangependa kujua maisha yako yakoje kwa sasa baada ya kuokoka na kuachana na mambo ya kidunia?
Pretty Kind: Kiukweli maisha yangu tangu nimpokee Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu, kwanza yamekuwa mazuri, nina amani tele, sina stress kama ilivyokuwa zamani na muda mwingi ninafanya maombi, nimeamua kuachana na machafu yote.
My Style: Umewezaje kuacha hayo machafu angali wewe ni msanii tena mwanamke mrembo?
Pretty Kind: Ni Mungu tu, ukimwomba na kumtegemea kila kitu kinawezekana.
My Style: Vipi ratiba yako kwa siku ikoje?
Pretty Kind: Nikiamka cha kwanza huwa ninasali kwanza baada ya hapo nashika simu yangu nawasiliana na ndugu na jamaa nikimaliza, natoka naenda zangu mitaani kufanya kazi zangu, lakini mara nyingi huwa nakuwa kanisani.
My Style: Shopping zako za nguo ni shilingi ngapi na unazifanyia wapi?
Pretty Kind: Shopping zangu ni za gharama ndogo sana kwani napenda kuvaa nguo full ambapo inanigharimu kuanzia shilingi laki mbili kwenda juu na huwa nanunua kwenye maduka makubwa kama Mlimani City.
My Style: Je, kwa siku unatumia shilingi ngapi?
Pretty Kind: Kwa siku ninatumia shilingi 80, 000.
My Style: Unapenda kujiachia viwanja vya aina gani vya starehe?
Pretty Kind: Sipendi kwenda kwenye kumbi za starehe kwa sababu sipendi makelele, napenda kukaa nyumbani na kujisomea Biblia.
My Style: Starehe yako hasa ni nini?
Pretty Kind: Starehe yangu ni kula, yaani napenda sana kula kwa kweli.
My Style: Zaidi unapenda chakula gani?
Pretty Kind: Napenda sana wali maharage tangu nikiwa mtoto.
My Style: Unapenda kuvaa nguo za rangi gani?
Pretty Kind: Napenda rangi nyeusi na nyekundu.
My Style: Je, ni nguo za aina gani unazozipenda?
Pretty Kind: Napenda suruali na nguo fupi maana zinanikaa vizuri zaidi.
My Style: Kwa nini unapenda nguo fupi wakati wewe ni mlokole?
Pretty Kind: Napenda suruali na vimini tangu nikiwa mdogo, nilikuwa nakata nguo nikinunuliwa ndefu.
My Style: Unaweza kununua nguo au viatu kwa gharama gani?
Pretty Kind: Kwa jinsi ninavyopenda kupendeza na nikiwa na fedha huwa nachukua nguo mpaka za shilingi laki sita.
My Style: Asante sana.
Pretty Kind: Karibu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments