RC Mwanri azitaka Taasisi za Fedha Kutoa Elimu Ya biashara kwa Wajasiriamali | ZamotoHabari.

Na, Editha Edward-Tabora 

Taasisi za fedha hapa nchini zimeshauriwa kutoa elimu ya biashara kwa Wajasiriamali wadogo ili biashara zao ziwe na tija na kuwainua zaidi

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipotembelea mabanda ya taasisi mbalimbali ikiwemo za kifedha na wajasiriamali wadogo katika viwanja vya maonesho ya nanenane katika manispaa ya Tabora

Pia amesema kuwa wajasiriamali wadogo wanamchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yoyote ile hapa duniani hivyo wanapaswa kupewa elimu itakayowasaidia kuimarisha biashara zao ipasavyo

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zilizoko mkoani humo kuwajengea uwezo Wakulima na Wafanyabiashara wadogo ili waweze kuinuka kiuchumi

Komanya ameendelea kusisitiza kuwa mabenki yana nafasi kubwa sana ya kuwainua Wakulima na Wafanyabiashara kutoka Kiwango cha chini hadi cha juu ikiwemo kuwawezesha kuanzisha viwanda vidogo vya kati na vikubwa 

Aidha amesema kuwa maendeleo makubwa tunayoyaona hapa nchini yanachochewa na kodi inayolipwa na Wafanyabiashara, hivyo akawataka Wafanyabiashara wakubwa wote mkoani Hapa kuwa na mashine za kielektroniki.
Pichani ni mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri Akizungumza na mmoja wa taasisi za Benki kuhusu kutoa elimu kwa wajasiriamali.
 Pichani  ni wafanyakazi wa taasisi za kibenki wakizungumza na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( pichani hayupo) .


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini