Serikali ya Kenya yaagiza Bar zote zifungwe wikiendi hii, Wakenya wageuka mbogo mtandaoni | ZamotoHabari.


Serikali ya Kenya imeagiza kuwa kuanzia Jumamosi Agosti 24 hadi Jumapili Agosti 25, 2019, Bar na kumbi za starehe zote nchini Kenya zifungwe ili kupisha zoezi la Sensa.


Amri hiyo imetolewa jana Agosti 21, 2019 na Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Kenya, Fred Matiang’i wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mashidano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Makampuni ya kutoa huduma ya maji nchini humo, Iliyofanyika katika uwanja wa Embu.

“Tunaenda kufunga mahali pote pa kujiburudisha kwanza tutaanza na Bar, Tutafunga kuanzia saa 11 jioni hadi 12 asubuhi ili kukupatia muda wa kuwa nyumbani kabla ya maafisa wa kuhesabu watu kufika majumbani kuanzia saa 12 jioni,” amesema Waziri huyo.

“Hakuna mtu atatoka nje ya kijiji chako, kumaanisha kuwa ni watu ambao wanafahamu kila mtu hapa, wanajulikana na wanajua kila mahali,” ameongezea Matiang’i.

Waziri huyo pia, Amewahakikishia Wakenya kuwa hali ya usalama itaimarishwa kwani maafisa wote wa usalama wamezuiliwa kwenda likizo ili kuhakikisha zoezi hilo linamalizika salama.

Matiang’i pia alitoa onyo kali kwa wale ambao watakuwa wanajifanya wasimamizi wa zoezi hilo bila idhini ya serikali, Kwa kudai kuwa asasi zote za kigeni na watu binafsi wamepata mafunzo maalum kabla ya kuidhinishwa.

Zoezi la kuhesabu watu litakuwa la siku mbili tu, Nalitaendeshwa kwa mfumo mpya wa kidigitali ili kuhakikisha idadi kamili ya Wakenya inajulikana.

Zoezi la Sensa nchini Kenya hufanyika kila baada ya miaka 10, Na kwa mwaka huu mtu yeyote atakayebainika kudanganya takwimu za familia atapigwa faini hadi ya Ksh 100,000 sawa na Tsh Milioni 2.2 .

Hata hivyo, Baadhi ya Wakenya hawajapokea taarifa hiyo kwa furaha, Kwani wamedai kuwa itazuia uhuru wa watu kutazama mipira kwenye Bar na kukosesha mapato kwa wafanyabiashara.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini