SERIKALI YAWAOMBA WADAU WA USAFIRI MIKOA YA KASKAZINI KUTOA MAONI YAO ILI KUIBORESHA RASIMU MPYA YA HUDUMA YA USAFIRI NCHINI | ZamotoHabari.

Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

SERIKALI imewaomba wadau wa huduma ya usafirishaji mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara kutoa maoni yao kwa ajili ya maboresho ya rasimu mpya ya huduma za usafirishaji nchini ili kuboresha kanuni za usafirishaji na yatafanyiwa kazi.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hagnes Chitukulo, alipokuwa akifungua kikao cha siku moja cha kujadili rasimu mpya ya kuboresha huduma ya usafiri iliyowasilishwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kinachoshirikisha wadau wa huduma ya usafiri ambao ni wamiliki wa mabasi, daladala, malori ,madereva, makondakta, bajaji ,taxi.

Chitukulo, amesema Serikali inatayaka kutunga sheria mpya ya huduma za usafiri, hivyo imeaandaa rasimu na kuipeleka kwa wadau ili watoe maoni ya kuiboresha na waweze kuboresha huduma za usafiri nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma ya uchukuzi, Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Haron Kisaka amesema rasimu hiyo mpya inalenga kuboresha huduma ya vyombo vya usafiri .

Amesema Wizara imetoa kanuni mpya za huduma ya usafirishaji na sasa rasmu hiyo inapelekwa kwa wadau ili waweze kuitolea maoni ili baadae itengenezwe sheria za usafiri wa ardhini ,ambazo sasa zitasimamiwa na LATRA.

Amesema Serikali imeanzisha mamlaka ya kusimamia huduma za usafiri wa ardhini ambayo ni LATRA inayochukua nafasi ya Sumatra ,ambayo ilikuwa inadhibiti huduma za usafiri wa barabara, leri na anga

Amesema kulingana na mabadiliko hayo wamiliki wa mabasi kuanzia sasa watakuwa wakitumia mfumo wa Kielektoroniki kutoa tiketi za mabasi na lengo ni kuboresha huduma na kuondoa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi ambao wamekuwa ni kero.

Kisaka amesema kuwa tayari yapo baadhi ya mabasi yameshaanza kutumia mfumo wa kutoa tiketi za abiria za kielektroniki na mfumo huo ni mzuri .

Kisaka, amesema sheria mpya namba 3/2019 inayodhibiti vyombo vyote vya usafiri nchini inawashirikisha, wamilikio, madereva,makondakta, magari ya kukodi yaani Taxi,bajaji

Katika hatua nyingine wadau wamegomea kikao hicho na kimemalizika bila maafikiano kutokana na kutokuelewana kati ya wadau na Serikali kutokana na hoja za wadau kutaka kupewa muda zaidi ili wakaisome rasimu hiyo .
Wadau wamedai kuwa wamechelewa kupata nakala za rasimu hiyo hivyo inawawia vigumu kuijadili kwa kuwa hawajaipitia na kuelewa na hivyo kusisitiza wapewe muda zaidi .

Huku upande wa Serikali ukisisitiza kuwa wanatakiwa kutoa maoni kwa kuwa tayari rasimu imeletwa kwao hivyo hawana budi kiuijadili na kuwataka watenganishe changamoto zao na utendaji kwa kuwa serikali itarejesha rasimu hiyo ili waweze kuipitia.

Kisaka, amesisitiza kwamba baadhi ya vyama vya watoa huduma walipokea rasimu hizo muda wa siku nne zilizopita kabla ya kikao hicho kulingana na kumbu kumbu zilizopo hivyo anawashangaa kudai hawajapata nakala hizo .

Mwenyekiti wa AKIBOA,Loken Masawe, akichangia ameomba wadau wa huduma ya usafirishaji kuwapa muda zaidi ili waisome rasimu hiyo wailewe waweze kutoa maoni yao ,na wasilazimishwe kwani hawana ugomvi na serikali .

Kwa upande wake mmiliki wa mabasi ya Mtei,Mwenyekitio wa TABOA Mkoa wa Arusha, Felix Mtei, rasimu ilichelewa kuwafikia wahusika ,wamiliki na madereva walitakiwea kufafanuliwa maeneo yanayowagusa.

Amesema kuwa kwa minajili hiyo wadau tunatakiwa walione suala hilo kwa Hivyo wanahitaji muda zaidi ili wafafanuliwe kisheria kuweza kujadili suala hilo kuweza kutoa maoni yao kuboresha rasimu hiyo kwa uwazi na muda.



Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini