Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ramadhan Nassib (kushoto) enzi za uhai wake akiwa na Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF
ALIYEWAHI kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ramadhan Nassib amefariki dunia alfajiri ya jana Alhamisi katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali zilizotoka jana zilieleza kuwa, Nassib alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kabla ya kukutwa na umauti. Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF, amethibitisha kifo hicho kwa kusema:
“Nimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Ramadhan Nassib, hakika ni pigo kubwa kwa TFF kwa kuwa bado alikuwa na mchango mkubwa kwenye mpira wa miguu.
“Kwa niaba ya TFF natoa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na wanafamilia wa mpira wa miguu.” Enzi za uhai wake, kiongozi huyo aliwahi kuongoza mpira wa miguu katika ngazi mbalimbali ikiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Kamati ya Utendaji na kamati mbalimbali za TFF. Innalilah Wainna Ilayh Rajiun.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo BOFYA HAPA
0 Comments