VIDEO: Alalamika Kurushiwa Mawe Yenye Moto juu ya bati, Mrushaji Haonekani | ZamotoHabari.



Mkazi wa kijiji cha Tindigani wilayani Siha mkoani Kilimanjaro anyejulikana kwa jina la Godfrey Nasary amesema amekuwa akirushiwa mawe kwa zaidi ya siku 20 bila kumuona anayerusha mawe hayo huku yakiharibu nyumba yake ikiwemo mabati pamoja na vioo.

Amesema wakati akiwa na wachungaji wanaomba wanashangaa mawe yanarushwa na kuna siku jiwe lilirushwa likiwa linawaka moto huku akihusisha suala hilo na mambo ya kishirikina.

“Sasa hivi ni wiki mbili na zaidi kwamba yaliibuka tu mawe yakirushwa juu ya bati, mawe ni makubwa ambayo yanarushwa nyakati za usiku. Siku nyingine yanaanza mchana kuanzia saa 11 mpaka kwenye muda wa saa tatu. Wachungaji wamekuwa wakifanya maombi na sisi pia huwa tunafanya maombi. Ukifika wakati wa maombi ndiyo kwanza wanachachamaa kurusha mawe.”

Amesema wamejaribu kufanya uchunguzi lakini mpaka sasa hawajagundua anayefanya tukio hilo, hivyo kuingiwa na hofu kubwa.

Amesema mawe hayo yameharibu sana mabati ya nyumba yake kiasi kwamba yamekuwa hayafai tena na ikiwa mvua itanyesha basi nyumba itakuwa ikivuja.

Amesema maeneo mengine ya nyumba ambayo yameathiriwa na mawe hayo ni madirisha na sehemu za milango ambazo zimenakshiwa na vioo.

Zaidi angalia video hii;

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini