Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha
Viongozi wa dini kote nchini wametakiwa kurejesha fadhila kwa waumini wao na kuwasaidia wananchi na watu wasio jiweza .
Hayo yamebainishwa na Nabii Mkuu Dr GeorDavie Wa huduma ya Ngurumo ya upako Jana wakati akigawa fedha za kuwaongezea mitaji baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo Wa eneo La Kisongo lililopo ndani ya halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru mkoani hapa.
Alisema kuwa viongozi wengi wadini wamekuwa hawarudishi fadhila kwa waumini wao ,huku wengine kusahau jamii inayowazunguka kitu ambacho ni kibaya kwani hata katika vitabu vya dini imeandikwa ,watu wasio jiweza , yatima na masikini wasaidiwe .
Aidha ametumia muda huo kumpongeza Rais Wa Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh John Magufuli kwa jinsi anavyofanya Kazi pamoja na jinsi anavyo wajali wanyonge na watu wasiojiweza huku akibainisha kuwa ataendelea kumuombea pamoja na kumuunga mkono katika juhudi za kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
" kutoa msaada huu ni njia moja wapo ya kumuunga mkono Rais wetu kwa Kazi nzuri anazofanya ,na tutaendelea kumuunga mkono ,Rais wetu ameonyesha njia ya kusaidia wanyonge na wasio jiweza na Mimi kama kiongozi Wa serikali ya ufalme wa mungu nimeamua kumuunga mkono na Leo sio mwanzo wala mwisho nitaendelea kutoa msaada kila Siku kadri mungu anavyo niongoza.
Alisema Katika serikali za duniani Wananchi wa Hali ya chini ndio wapiga kura na ndio walipa Kodi, vilevile katika serikali ya ufalme wa mungu wao ndio watoji wa kubwa wa sadaka na matoleo mbalimba, alisema wakiwezeshwa watafanya zaidi ya jinsi wanavyofanya Sasa katika serikali zote mbili
Nabii huyo ametoa zaidi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuwaongezea mitaji wajasiriamali wadogo Wa eneo La kisongo ikiwa Ni muendelezo wa kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo ambao kwa mwaka huu ametoa Zaidi ya milioni 200, ikiwa Ni pamoja na kuwajengea nyumba watu wasio nauwezo, kuwapa vijana pikipiki za biashara (bodaboda) pamoja na kutoa magari kwa watu mbalimbali huku akiahidi kutoa pesa na Mali kwa watu wengine kadri Mungu atakavyo muongoza .
Wakiongea Mara baada ya kupokea msaada huo Wa mitaji baadhi ya wajasiriamali wamemshukuru Nabii Mkuu kwa kuwawezesha kibiashara huku wakisema utawasaidia kukuza biashara zao.
"Kwakweli namshuru Mungu kwa kutuletea Huyu baba, Mimi nilikuwa na mitaji Wa machugwa Wa elfu kumi nimepewa hii laki moja kwa kweli nashukuru ,kwani sitauza machugwa tena Bali nitabadilisha biashara na nitaanza kuuza dagaa nashukuru sana" alisema Mary Kristofa
Kwa upande wake Marieta Daudi amemshukuru kwa msaada huo na kuwataka viongozi wengine Wa dini kuwa na moyo huo Wa kutoa ili kuweza kuwainua wananchi Wa chini na wasio jiweza.
Nabii Mkuu Dr GeorDavie Wa huduma ya Ngurumo ya upako akiwa anampa msaada Wa fedha mama mmoja mfanyabiashara Mdogo kwaajili ya kuongeza mtaji
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments