WANAWAKE WAPEWA KIPAUMELE SIKU YA UBINADAMU DUNIANI | ZamotoHabari.

Mwanamke ambaye anayefanya kazi ya ubinadamu inchini 'Nigeria katika Mfuko wa ubinadamu, Adamawa State amaye anatoa huduma kwa mama mjamzizito nchini Nigeria. 

Na Mwandishi wetu
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ubinadunia ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Agosti 19, ni siku ambayo walimwengu hukusanyika katika maeneo mbalimbali kuadhimisha na kuwapongeza watu wote waliojitolea nafsi zao kuokoa wanadamu wenzao na kufanya jitihada za kuifanya dunia hii kuwa mahala pa amani na usalama zaidi pa kuishi. 

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa, António Guterres amesema kuwa 
"Tusaidie raia walio patwa na majanga au shida (crisis) hasa mlipuko wa magonjwa kwa binadamu hasa wanawake wakipewe kipaumbele wananwake ili kuwapa msaada wa kibinadamu kwa kujali utu kwanza". 

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Guterres  amesema kuwa watu wanaofanya kazi za kijamii kwaajili ya binadamu waliopatwa na majanga hasa watu waliojeruhiwa katika mapigano ya vita nchini Afghanistan na watu waliopata majanga ya ukosefu wa chakula, hasa nchi za Afrika ya kati, Sudani Kusini, Syria, na Yemen zenye balaa la njaa wanahitaji msaada wa kibinadamu.


Hata hivyo wanawake 
duniani kote wanatakiwa  kupongezwa kwani shughuli wanazozifanya zinatoa  msaada wa kibinadamu.

Amesema wanawake Wanawake wanatakiwa kusheherekea siku ya ubinadamu duniani kwa kuwa ndio wanaojitolea maisha yao katika kuokoa maisha ya watu wengine duniani kote.

Aidha watu wote wanatakiwa kuokoa maisha ya watu wengine ili dunia iwe mahali salama pakuishi kulingana na sheria za kimataifa katika kutetea uhai wa binadamu. 


Siku hii ya ubinadamu duniani ilianzishwa kwaajili ya kuunga mkono na kuendeleza juhudi za kusaidia binadamu waliopatwa na majanga au shida mbalimbali duniani kote.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini