Wolper Ahofia Kupigwa Juju | ZamotoHabari.

BAADA ya kuonekana akiongea bila breki, staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amesema siku hizi anaona mdomo wake hauna staa mpaka anahisi utapigwa juju. 

Akizungumza na Za Motomoto ya Risasi, Wolper alisema anajishangaa kwa nini siku hizi akipewa kipaza sauti maneno yanatoka bila hata kupiga kituo.

“Unajua baada ya kumaliza kuongea siku zote nikisikiliza najiuliza mdomo wangu una nini, ingawaje nakuwa katika hayo maneno nimeongea ukweli kabisa, inafika wakati mpaka nawaza watakuja kuupiga juju uende upande,” alisema Wolper
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini