BARAZA LA JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM CHATO WAHAMASISHWA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA | ZamotoHabari.

Na Editha Karlo wa Michuzi Tv,Chato

BARAZA la Jumuiya ya wazazi wa chama cha apinduzi(CCM) WilayaniChato wamehamasishwa kujiunga na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu wanapougua wao na familia zao.

Meneja wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Geita Elias Odhiambo aliwaambia wajumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Chato kuwa ni muhimu kujiunga na bima ya afya wamehamasishwa kujiunga na Bima ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu na dawa pale wanapougua hata kama hawana pesa mfukoni.

"Ugonjwa huwa unakuja bila ya taarifa,unaweza kuugua mfukoni huna hata pesa,lakini unapokuwa na kadi yako ya bima ya afya unakuwa na uhakika wa kupata matibabu na dawa"alisema Odhiambo

Odhiambo aliwaomba wajumbe hao kujiunga na Bima ya Afya kwa uhakika wa matibabu pia ilani ya Chama Tawala inaelekeza wananchi kujiunga na Bima ya afya.

"Mkiwa kama wasimamizi wa ilani ya chama tawala niwaombe mjiunge na utaratibu wa Bima ya Afya, Kwani sasa wananchi wanawigo mpana wa kujiunga na Bima ya afya kupitia NHIF au CHF iliyoboreshwa"alisema Meneja

Alisema kuwa upande wa NHIF zipo huduma mbalimbali za bima kama Bima kwa watumishi, Ushirika Afya kwa Wakulima, Bima kwa Watoto na Wanafunzi,Vile vile hivi karibuni NHIF itaanzisha mpango wa Bima ya Afya kwa mtu mmoja mmoja.

Odhiambo aliongeza kwa kusema kuwa kujiunga na Bima ya Afya ni kuwekeza kwenye afya yako ili kukabiliana na changamoto ya ugonjwa kuja bila hodi na gharama kubwa za tiba. 

Amewaomba wajibu hao kupitia kauli yao ya uchungu wa mwana aujuaye mzazi kwa kujiunga na Bima ya afya sambamba wananchi wengine kujiunga na Bima ya afya.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Chato Acheny Mwinshehe Maulidi amewaambia wajumbe hao umuhimu wa Bima ya Afya akitolea mfano wa jinsi ambavyo yeye na familia yake wamekuwa wanufaika wa NHIF. 

Katibu huyo ameahidi kuwa balozi wa kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini