Hali ya Mchekeshaji Kevin Hart Baada ya Kupata AJALI Mbaya ...Afanyiwa Upasuaji | ZamotoHabari.



Star wa filamu na vichekesho nchini Marekani amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa mgogo baada ya kupata ajali mbaya ya gari mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Malibu hills.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40 alipata ajali hiyo akiwa na gari yake aina ya Plymouth Barracuda huku ndani ya gari hilo kukiwa na watu watatu lakini mmoja hakupata tatizo lolote japokuwa gari iliharibika vibaya.

Mke wa msanii huyo Enika Hart amethibitisha mume wake huyo kufanyiwa upasuaji wa sehemu ya mgongo na sasa anaendelea vizuri.

‘Tunashukuru kevin anaendelea vizuri kwasasa aalifafanikiwa kufanyiwa upasuaji sehemu ya mgongo na hali yake kwa sasa imeanza kukaa sawa, tunashukuru kwa maombi na salamu mbalimbali za pole kupitia mitandao ya kijamii’ alisema Eniko.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini