Sanaa imezaliwa upya, lakini hii ni yetu sote ni semi ambazo zilitumika na zinatumika tangu uzao wa Wasafi Radio na Runinga. (Hakika)
Na mwanzo kila mmoja alipata tumaini juu yao, kadhalika wajuzi tulijua yakuwa hakuna uhalisia bali kuvutia usikivu na utazamaji. (Tafakari)
Ambapo lugha kali zikatawala mno kwa vyombo vingine juu ya kuonekana ni wabaguzi
kwa kuacha kucheza kazi ya wasanii fulani.(Naam)
Na Wasafi kuonekana wao ni wenye kucheza wasanii wote bila ubaguzi. Ingawaje haikuwa kweli bali unafiki ambao unapaswa uwe mjuzi ili uweze kutambua. (Uhalisia)
Tuwe wa kweli mzunguko anaopata Queen Darlin ni sawa na mzunguko wa anaopata Mwasiti au Linah au msanii mwingine yoyote katika usikivu wa Wasafi? (Ulizo)
Ikumbukwe hata kujiengua kwa Rich Mavoko toka Wcb je! aliendelea kupata upana wa mzunguko kama ilivyokuwa awali? (Thubutu)
Uhalisia ni kwamba kucheza wimbo na kuupa mzunguko ni viwili tofauti. Mzunguko ni ile wimbo kuchezwa mara nyingi zaidi kwa maana kila baada ya muda fulani unarudiwa. (Eeh)
Je! Wasafi hufanya hivyo katika wasanii wapi au nyimbo zipi? Si zile ambazo ziko na maslahi yao. (Kabisa)
Na juzi ya Harmonize katika kutaka kujiengua ama kujiengua na Genge hilo, je! anapata mzunguko Wasafi? (Aah Wapi)
Na jana ya ndoa yake waliweze kuripoti kama vyombo vingine vya habari vilivyoripoti? Ni wazi ni ukimya tawala kama hakuna alichofanya. (Hapana)
Hii inatuonyesha wazi yakuwa hata wao ni kama wale ambao walikuwa wakiwatolea lugha kali huku wakiiga kila jambo toka kwa wale. (Clouds)
Wasanii na mashabiki wanapaswa wajue yakuwa kila chombo kinacheza wimbo kwa maslahi makuu, kama hauna maslahi nao na kuwa tofauti tarajia kuwa nje ya mfumo. (Uhalisi)
Vivyo hakuna mwenye nafuu katika vyombo vya habari juu ya msanii bali maslahi kulingana na maelewano yenu. (Faida)
Vivyo Wasafi ni kama wengine tu, hakuna ambaye atabeba sanaa yote bali maslahi kamili yenye ujazo kwake na kwako msanii. (Tafakari)
#MuzikiNiSisi
Post Views: 1,488
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments