Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapoa kihutubia wakati wa uzinduzi wa Awamu ya pili ya Mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe.
Balozi wa Ubelgiji Nchini Tanzania Mhe, Balozi. Peter Van Acker akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe.
Wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kuzindua rasmi awamu ya pili ya mradi.ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo (katikati Kushoto mwenye suti nyeusi), Mhe, Balozi. Peter Van Acker katikati kulia mwenye tai nyeusi), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ugent na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe (wenye sare ya batiki kulia na kushoto)na waratibu wa mradi kwa Tanzania na Ubelgiji.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr.Leonard Akwilapo (kulia) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Mohammed Utali wakiwasili Chuo Kikuu Mzumbe kwenye sherehe za uzinduzi awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4.
Baadhi ya washikiri wa sherehe za Uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa Vlirous P-4 Chuo Kikuu Mzumbe.
Mratibu wa Mradi wa Vlirous wa nchini Ubelgiji Pro Koen, akielezea malengo ya mradi na mipango ya utekelezaji kwa awamu ya pili, wakati wa uzinduzi Chuo Kikuu Mzumbe.
KATIBU Mkuu Wizaraya Elimu, Sayansina Teknolojia Dr. Leonard Akwilapo leo amezindua awamu ya pili ya mradi “VLIROUS P4”unaofadhiliwanaSerikaliyaUbelgijikupitia Chuo KikuuUgent.
Kuzinduliwakwaawamuya pili ya mradi huo kumetoka na na mafanikio makubwa ya awamuya kwanza ya mradi ambapo jumla ya miradi minne imetekelezwa ikiwemo ufadhili ya masomo kwa wanafunzi wa ngazi ya shahada ya Uzamili, Shahada yaUzamivu, Tafiti mbalimbali na huduma kwajamii.
Akizundua mradi huo Katibu Mkuu Akwilapo amepongezana kushukuru Serikali ya Ubelgiji kwa ufadhili wa miradi mbalimbali sekta ya Elimu, na kuahidi Wizara yake kuendelea kuisimamia ili kuwa na matokeo ya nayotarajiwa katika ustawi wa Chuo na Maendeleo ya jamii kwa jumla.
Amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe kuendelea kutekeleza malengo ya Mpango Mkakati wake wa miaka mitano kwa vitendo kwa kuimarisha na kuinua viwango vyatafiti, na kutumia vizuri fursa zilizopo kuimarisha ubora na kiwango cha elimu kina chotolewa chuoni hapo.
Naye balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Mhe. Balozi Peter Van Acker amesema matarajio yake ni kuona namna Vyuo Vikuu vinavyoweza kuhusianishwa moja kwa moja na maendeleo ya jamii kupitia miradi ya maendeleo kama huu wa Vlirous, na kuahidi Serikali ya Nchi yake kuendelea kufadhili miradi mingi zaidi ya Elimu nchini Tanzania.
Akitoa salamu za Chuo Kikuu Mzumbe, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano kusiluka amesema mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa husani katika kuonyesha kiuhalisia mchango wa Vyuo Vikuu katika maendeleo ya jamii, na kuunga mkono jitihada za Serikali kufikia uchumi wa viwanda.
Awamu ya kwanza ya mradi imeleta mabadiliko makubwa katika matumizi ya Teknolojia ndani ya Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na kubuni mifumi ya Tehama katika kutatua changamoto ya Afya, Ujenzi wa kituo cha kuchakata malighafi ya asali Turiani, kutoa mafunzo ya mbinu za ujasiriamali kwa wananchi wa Wilaya ya Mvomero, mafunzo kwa walimu wa Sekondari kuhusu mbinu bora za ufundishaji n.k
Uzinduzi huo umekwenda sambamba na uwasilishaji wa mafanikio na changamoto za kila mradi pamoja na kuonyesha washiriki matokeo ya tafiti zilizofanyika.
Mbali na kuzindua awamu ya pili ya mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipata fursa ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa eneo la Maekani unaofadhiliwa na Serikali.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments