KONGAMANO LA KIBIASHARA KUFANYIKA JIJINI DAR | ZamotoHabari.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda.
Mratibu wa Kongamano la biashara baina ya Tanzania na Uganda Ali Gugu akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema Jijini Dar es salaam

Na Mwandishiwetu             
WAZIRI wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza Kwa wingi kushiriki katika kongamano la biashara la Tanzania na Uganda linalotaraji kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo Jijini hapa Bashungwa amesema kongamano hilo ambalo litafunguliwa na kuhudhuliwa na wakuu
 wa nchi zote Mbili Tanzania na Uganda.

"Rais Magufuli amemualika Rais Museveni  wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano hii ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 1000 ambao  watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza  biashara mpya baina ya nchi hizi Mbili" amesema Waziri Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze kupata mtandao mpya wa kibiashara.

Ametaja muungano wa kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila uchwao.

Ametaja muungano wa kibiashara baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa nchi yetu ya Tanzania kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi kwao kuliko wao kuuza kwetu.

Amesema kuwa Uganda imekuwa ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa nafaka na Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri kwa kutanua masoko yao.

Amemaliza kwa kutoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza Kwa wingi katika kongamano hili.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini