MBUNGE MGIMWA KUTATUA KERO YA MAJI KIJIJI CHA IHANZUTWA | ZamotoHabari.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa sambamba na diwani wa kata ya Sadan wakati akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Ihanzutwa kwenye ziara ya kawaida jimboni 
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Sadan wakifurahia ujenzi wa ubora uliojengwa katika darasa la shule ya msingi Ihanzutwa kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Hili ni moja kati ya madarasa yaliyojengwa kwenye ubora wa hali ya juu kwa kupitia ufadhili wa TANAPA
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akifurahia jambo na watoto wa kijiji cha Ihanzutwa mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Wananchi wa Ihanzutwa wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ihanzutwa na kukosekana kwa maji safi na salama katika kijiji hicho hivyo wamemuomba mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini kusaidia kutatua kero hizo.

Wakizungumzana kwenye mkutano wa hadhara,wananchi hao wamesema kuwa wanashukuru kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini bado wanakabiliwa na ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasani katika shule hiyo.

“Sambamba nashukrani za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi za walimu na ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa kwa fedha za serikali lakini bado tunaomba kusaidiwa ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani” walisema wananchi 

Aidha wananchi wa kijiji cha Ihanzutwa walisemakuwa wanakabiriwana uhaba wa maji kwa miaka mingi hali inayosababisha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta maji hivyo walimuomba mbunge wa jimbo hilo kuwatafutia njia ya kutatua tatizo hilo

Akijibu maswali ya wananchi mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa amesema kuwa ameipokea changamoto hizo na atazifanyia kazi kwa kushirikianana wadaumbalimbali.

“Leo nikitoka hapa nitaendeleza mazungumzo na TANAPA ili waendelee kutusaidia kama ambavyo wametusaidia katika ujenzi wa madarasa na madarasa yaliyojengwa katika kijiji hiki huwezi kuyapata kijiji chochote kile kwa kuwa wanaubora wa aina yake” alisema Mgimwa 

Aidha Mgimwa amesema kuwa amewapata wadau ambao watasaidia kutatua kero ya maji kwakuchimba kisima kimoja katika kijiji hiki cha Ihanzutwa.“Tunamarafiki zetu wa Water For Africa ambao wametuahidi kutuchimbia kisima kimoja kirefu kwa lengo la kutatua changamoto hii ya maji katika kajiji hiki” alisema Mgimwa


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini