Mchekeshaji Kevin Hart Apata Ajali Mbaya ya Gari | ZamotoHabari.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Kevin alikuwa akijaribu kukwepana na gari jingine na hatimaye gari lake kuacha njia na kuangukia katika eneo la karibu na Maliba Hills California nchini Marekani. Hali ya kiafya ya mchekeshaji huyo ni nzuri na bado anaendelea kupatiwa matibabu.

Kevin Hart ameripotiwa kuumizwa vibaya mara baada ya kupata ajali mbaya ya gari jana Jumapili. Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Hart alikuwa akiendeshwa, ghafla dereva wake alishindwa kulimudu gari hilo na kuparamia kingo ya barabara mjini Malibu Hills.

Polisi wametanabaisha kuwa kulikuwa na watu wengine wawili kwenye gari. Pia Hart na dereva wake wameumia zaidi maeneo ya mgongo. Moja ya watu wake wa Ulinzi walimkimbiza nyumbani lakini baadaye alifikishwa hospitali kwa matibabu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini