Kwa mujibu wa Nyakati.com, baadhi ya wafuasi wao mitandaoni walishangaa ni vipi nyota huyo alifanya harusi kisiri pasi na hata kuwaalika wasanii tajika kutoka Tanzania. Hata hivyo, meneja wa Harmonize, Mjerumani amepinga kwamba wawili hao walifunga ndoa na kusema kwamba Sarah alikuwa akiigiza katika wimbo ambao staa huyo anatarajia kuutoa hivi karibuni
"Harmonize hakufunga ndoa Jumamosi iliyopita, ila alimshirikisha mpenziwe kwenye video ya wimbo wake atakaoutoa hivi karibuni wa 'Marry Me'. Wazo nzima la wimbo huo ni sawia na lile Diamond alitumia na kumshirikisha Zari katika wimbo wake wa 'Iyena'," Mjerumani aliliambia Nyakati.comItakumbukwa kwamba Aprili 2, 2019 Harmonize ambaye jina lake rasmi ni Rajab Abdul Kahali alimposa barafu wa moyo wake Sarah mwenye asili ya Kiitaliano nchini kwao Italy.
Harmonize mwenye umri wa miaka 25 alianza uhusiano wa kimapenzi na Sarah 2017, muda mfupi baada ya staa huyo kutengana na mchumba wake Jacqueline Wolper.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments