Mfalme wa Saudia amtumbua Waziri wa Nishati, Ampa nafasi mwanawe | ZamotoHabari.



Mfalme Salman wa Saudi Arabia amemuondoa katika wadhfa wake waziri wa nishati na kumpa nafasi hiyo mwanawe, aitwae Mwanamfalme Abdulaziz bin Salman.

Nafasi ya uwaziri wa nishati, ni moja kati vyeo muhimu katika taifa hilo la kifalme. Khalid al-Falih ameondoshwa katika nafasi yake ikiwa ni siku chache baada ya kupoteza nafasi yake kama mwenyekiti wa bodi ya kampuni kubwa ya mafuta ya serikali iitwayo Aramco.

Al-Falih vilevile alishuhudia hadhi yake ikipungua juma lililopita pale ambapo iliundwa wizara mpya ya madini na viwanda, na kuiondoa sekta hiyo kutoka katika uangalizi wa wizara ya nishati.

Waziri mpya wa Nishati Mwanamfalme Abdulaziz na waziri wa zamani wa nchi na masuala ya nishati Mwanamfalme Mohammed bin Salman ni ndugu wa baba mmoja. Inaaminika ndugu hao wawili hawana uhusiano wa karibu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini