Nigeria kutuma ndege 'kuokoa' raia wake Afrika Kusini | ZamotoHabari.


Raia wa Afrika Kusini wanawatuhumu wageni kwa kuchukua nafasi zao za ajira na kipato
Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini wamepewa ofa ya ndege za bure kurejea nyumbani kukwepa vurugu za kibaguzi zinazoendelea Afrika Kusini.

Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeri imesema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa.

"Wote watakaotaka huduma hiyo wanashauriwa kuwasiliana na Ubalozi wa Nigeria jijini Pretoria na ofisi ndogo za ubalozi jijini Johannesburg jwa matayarisho muhimu," taarifa ya wizara imeeleza.


Mashambulizi ya biashara zinazomilikiwa na wageni nchini Afrika Kusini zimepokelewa kwa hasira kali na Wanaigeria ambao wanahisi wanalengwa na kuonewa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama amewaambia wanahabari siku ya Jumatano kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea.

Hata hivyo, amesema kuwa serikali inaangalia uwezekao wa kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Afrika Kusini na kudai fidia kwa biashara zote za raia wa nchi hiyo zilizoshambuliwa.

Nigeria imesusia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi unaofanyika Afrika Kusini kutokana na ghasia zinazoendelea.

Serikali ya Nigeria tayari imeshatoa onyo kwa rai wake waliopo Afrika Kusini wakiwataka kutosafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

Haki miliki ya pichaAFP
Image caption
Waandamanaji nchini Nigeria wamevamia biashara za makampuni ya Afrika Kusini kulipiza kisasi
Mashambulizi ya kulipa kisasi kwa makampuni ya Afrika Kusini yaliyowekeza Nigeria pia yamefanyika, hali iliyoilazimu kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu- MTN - kufunga vituo vyake vya biashara kote nchini Nigeria.

Mwanzoni mwa wiki Raisi Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza 'ghadhabu' zao juu vurugu zinazoendelea.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini