RC Makonda awasilisha muswada wa marekebisho ya sheria ya mirathi | ZamotoHabari.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga muswada wa mapendekezo wa marekebisho ya sheria ya mirathi kwa ajili ya kufanyiwa maboresho na kuwasilishwa bungeni.

Muswada huo umewasilishwa jijini Dodoma na kuzitaja sheria kandamizi ambazo angependa zifanyiwe marekebisho kuwa ni pamoja na Sheria ya kiserikali ya mirathi, Sheria ya Mirathi ya Kimila pamoja na Sheria ya Mirathi ya Kidini kwa madai ya kuwa zimepitwa na wakati na zimekuwa zikileta mateso kwa wajane.

Makonda amekuwa akipigia kelele yafanyiwe maboresho pamoja na kipengele cha kumpa uhalali mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala mali kuhamishwa, pamoja na usawa wa watoto.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga, amesema kuwa alichokifanya Makonda ni ushujaa wa hali ya juu na ameweka historia ya jambo ambalo halijawahi kufanyika na kuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini