Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Ezamo Maponde amesema serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele kuwezesha mkakati wa maendeleo ya sekta binafsi katika nchi za Afrika Mashariki (PSDS) kufanikiwa.
Aidha alisema, serikali imekuwa mstari wa mbele kufanya mabadiliko mbalimbali ya sera zake ikiwemo mpango wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2015 ili kusukuma mbele sekta za Kilimo na biashara.
Alisema hayo wakati wa kufunga kwa mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki , mradi uliokuwa ukiratibiwa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Sera, Uratibu na Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu alisema kutokana na mabadiliko ya kisera na usimamizi wa utekelezaji wake Tanzania imefanikiwa kujiondoa katika utegemezi.
Alisema juhudi zilizofanyika kuweka msingi katika mradi huo kutatochoea kuimarishwa kwa Kilimo na kuwa na Kilimo biashara ili ndoto za kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda kufanikiwa.
Alisema kutokana na haja hiyo serikali imekuwa ikitengeneza sera na kubadili kanuni mbalimbali ili kuhimiza uchumi wa kiushindani wa viwanda toka mwaka 1961 kwa lengo la kupunguza utegemezi katika bajeti. Sekta ya viwanda nchini imegawanyika katika maeneo matatu ya uzalishaji (53%) uchakataji (24 %) na uunganishaji (4%).
Kwa kuwa uchumi wa Tanzania unategemea mazao ya Kilimo kinachoajiri asilimia 75 ya wananchi, ndio nguzo ya uzalishaji wa bidhaa katika viwanda.
Kutokana na utegemezi huo viwanda vinavyochakata mazao ya Kilimo hasa chakula ni asilimia 24, viwanda vya nguyo na nyuzi asilimia 10 na kemikali asilimia 8.5.
Akizungumzia mradi huo Profesa Fortunata Makene, Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) alisema kwa kiasi kikubwa umesaidia katika kuleta tija katika sekta ya kilimo na biashara ikiwemo kuzishawishi serikali kufanya mabadiliko katika sera zake.
Akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara kujadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, alisema mradi huo uliokuwa na lengo la kuzishawishi serikali katika masuala ya sera kupitia mpango ujulikanao kama 'National Reference Group'.
Alisema mradi huo ulilenga kuangalia namna ambavyo masuala ya mabadiliko ya tabia nchi yanahusishwa na shughuli za kilimo na biashara ili kuleta tija kwa wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.
Profesa Makene alisema kimsingi mradi huo uliondeshwa kwa awamu mbili kwa vipindi vya miaka minne minne tangu kuanzishwa kwake umeweza kuchangia mabadiliko hayo na kuongeza uelewa kwa wadau husika wakiwemo wanawake kutoka vikundi mbalimbali vinavyojishughulisha na kazi za usindikaji wa vyakula na bidhaa
Aidha alisema uwepo wa sera madhubuti katika kilimo na biashara kwa kiasi kikubwa kumeweza kuleta mabadiliko chanya kwa wakulima na wafanyabiashara ikiwemo kuongeza thamani katika mnyororo.
Nchi za Afrika Mashariki kwa sasa zipo katika kuendeleza mpango wa Private Sector Development Strategy (PSDS) 2018-2022 wenye lengo, la kuimarisha mazingira bora ya biashara na kuzifanya kuwa za ushindani.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Ezamo Maponde akizungumza wakati wa kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) katika hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dk. Tausi Kida wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Ezamo Maponde (kulia) na Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene wakiwa meza kuu wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtafiti mwandamizi wa ESRF Dk. Hoseana Bohela Lunogelo akizungumzia nafasi ya wadau katika mchakato wa PSDS wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Tanzania kwenye Shirika la Biashara Duniani (WTO) jijini Geneva , Uswis Bi. Neema Manongi akizungumzia kinachotarajiwa kutoka WTO za utengenezaji wa mnyororo wa thamani kwa bidhaa za mashambani wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Dk Ladislaus Chang’a, kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) akiendesha majadiliano kuhusu namna ambavyo mazungumzo ya kimataifa kuhusu biashara na mabadiliko ya hali ya hewa yalivyochagiza uumbaji wa sera zinazotumiwa na serikali kuwezesha uchakataji wa bidhaa za kilimo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa programu CUTS International, Nairobi Bw. Collins Owegi akizungumzia nini kilichofanyika na kufanikiwa katika PACTEAC2 wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa kitaifa wa TCSAA ambaye pia ni mshiriki majadiliano ya UNFCCC Bi. Shakwaanande Natai akizungumza kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na uhuishaji wake kwenye kilimo chini ya makubaliano ya Koronivia wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Dk. Donatilla Kaino wa ESRF akiendesha majadiliano ya mada kuhusu mradi PACTEAC 2 ambapo yaliangalia uwezeshaji uliofanyika na kipi kitaendelea wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha utafiti mkakati na machapisho kutoka Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akifafanua jambo wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadh ya wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara wakishiriki kutoa maoni wakati wa hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara walioshiriki hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wadau mbalimbali wakiwemo watafiti wa masuala ya kiuchumi, wakulima na wafanyabiashara walioshiriki hafla ya kufunga mradi wa miaka nane wa uhamasishaji kilimo, biashara pamoja na masuala ya tabia nchi katika nchi za Afrika Mashariki (PACTEAC 2), mradi uliokuwa ukiratibiwa na ESRF ambapo pia walijadili matokeo ya mradi huo awamu pili tangu kuzinduliwa kwake, iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments