Serikali yaombwa kurekebisha mtaala Wa elimu ufundi stadi | ZamotoHabari.

Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya elimu ya ufundi stadi pamoja na kufanya marekebisho ya mtaala Wa elimu ya ufundi stadi kwani mtaala huo ni Wa zamani na unawapa changamoto kubwa walimu wanaofundisha shule hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Wa shule ya msingi ya Healsun  ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Elimu  ya Sinoni Edward Laiza wakati akisoma hotuba yake katika mahafali ya nne ya kidato cha saba ya shule hiyo.

Alisema kuwa mtaala wa elimu ya ufundi stadi haujaboreshwa tangu ulipotugwa mwaka 1984, hivyo unawapa tabu sana ya kupata vitendea Kazi ikiwemo vitabu vya kufundishia masomo mbalimbali  .

"Tunapata tabu sana kupata vitabu pamoja na vitendea Kazi vingine kwa sababu  mtaala huu haujarekebishwa tangu mwaka 1984, hivyo tunaiomba serikali kupitia mtaala huu na kuubadilisha ili tuweze kufundisha watoto kulingana na mtaala unaoenda na wakati kufanikisha Sera hii ya viwanda " alisema 

Alisema kuwa iwapo ufundi ukipewa kipaumbele itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira hapa nchini kwani ,wanafunzi wengi wanao maliza katoka shule hizi za ufundi watakuwa na ujuzi Wa kutosha Wa vitendo ambao watakuwa wametoka nao mashuleni  na wataweza kujiajiri wenyenyewe na sio kutegemea ajira za serikalini.

Kwa upande wake  mgeni rasmi katika Mahafali hayo Mwenyekiti Wa umoja Wa wazazi mkoa wa Arusha,  Daudi Hezron Mbise aliwatala wanafunzi hao kuzingatia na kuyafuata yale yote ambayo wamefundishwa na walimu wao ,huku akiwasihi kuhishika sana elimu na kuendelea kusoma  kwani kwa dunia ya sasa hivi elimu ndio kila kitu.

"Najua mmefundishwa vyema na walimu wenu sasa kazingatieni yote mliofundishwa darasani na hata nje ya darasani ,pia napenda kuwasisitiza wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni na sio kuwaachia walimu tu,  kwani ukifuatilia maendeleo ya mtoto kama yupo chini utajua jinsi ya kumkazania  mtoto wako.

Haya ni mahafali ya nne ya darasa la saba tangu kuanzishwa kwa shule hii mwaka 2014 na jumla ya wanafunzi 15 wamemaliza masomo yao ya darasani la saba  ,pia shule hii ina sekondari ya ufundi stadi inayofundisha masomo ya ufundi stadi lakini pia shule hii ya msingi  inatarajia kuanza kufundisha masomo ya ufundi stadi ili kuwasaidia wanafunzi .

Mkurugenzi Wa shule ya msingi ya Healsun ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Wa taasisi ya Elimu ya Sinoni Edward Laiza akisoma hotuba katika mahafali ya darasa la saba katika shule hiyo
wanafunzi Wa shule ya sekondari ya ufundi stadi Healsun wakionesha wazazi wao hawapo pichani ufundi waliofundishwa darasani kwa vitendo 


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini