Spika Ndugai Atangaza Utaratibu Mpya Kwa Wabunge | ZamotoHabari.

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amesema Bunge lina mpango wa kuacha kutumia mfumo wa sasa wa makaratasi Bungeni, kwa ajili ya kuwapa Wabunge nyaraka mbalimbali, watakachofanya sasa ni kuhamia katika mfumo wa Digitali, kwa kuwawekea kupitia kwenye simu zao.

Ndugai amesema kuwa Bunge hilo ndio pekee linalotumia makaratasi, kwamba mabunge mengine yameshaachana na utaratibu huo.

"Sisi ndiyo Bunge pekee Afrika Mashariki ambao tunaendekeza Makaratasi mengi, wenzetu hawatumii, tunaanza na hii 'Order Paper' halafu tutaenda kidogo kidogo

Amewataka wabunge kuthibitisha namba zao za simu wanazozitumia katika mtandao wa WhatsApp na email kwa ajili ya kuanza kupatiwa orodha ya shughuli za Bunge kwa siku husika kwa njia ya mtandao.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini