TCL ipo tayari kumsafirisha bure anayepumulia mashine | ZamotoHabari.



Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesema lipo tayari kumlipia gharama za usafiri mgonjwa anayepumulia mashine, Hamad Awadh (28) kutoka jijini Dar es Salaam hadi Mumbai, India ikiwa atapangiwa na madaktari kutibiwa katika mji huo.

Shirika hilo litatoa tiketi mbili za ndege kwenda India na kurudi Tanzania.

Hayo yameelezwa ikiwa zimepita siku tano tangu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuahidi kutoa Sh11.5 milioni, Sh10 milioni zikiwa kwa ajili ya matibabu na Sh1.5 milioni kumsaidia gharama za umeme.

Akizungumza na mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema watagharamia usafiri wa kwenda na kurudi.

“Tumempatia masharti yetu kwa kuwa ATCL inakwenda Mumbai India, tutamsafirisha iwapo atapata hospitali iliyopo Mumbai ili iwe rahisi kwake katika usafiri kwa maana tutamfikisha pale na tutaweza kumrudisha bila shida yoyote kwa gharama zetu,” amesema Matindi.

Awadh amelieleza Mwananchi kuwa tayari watu mbalimbali wanampigia simu wakitaka kujua gharama za matibabu nje ya nchi, lakini inakuwa vigumu kuzitoa kwani hajafanikiwa kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili – Mloganzila kufanyiwa upya vipimo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini