Timu ya Taifa ya vijana ya kuogelea imeondoka nchini kwenda Tunisia kushiriki katika mashindano ya Afrika ya kuogelea.
Timu hiyo inajumuisha jumla ya waogeleaji wanne ambao ni Yuki Omori anayetokea klabu ya Mis Piranhas ya mkoa wa Morogoro, Khaleed Ladha (Mwanza), Aaron Akwenda (Bluefins) na Mohameduwais Abdullatif wa klabu ya Taliss-IST.
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal alisema kuwa waogeleaji wapo tayari kuiwakilisha nchi
Katika mashindano hayo ambayo yatajumuisha waogeleaji zaidi ya 1000 kutoka bara la Afrika.
Alisema kuwa waogeleaji hao wamechaguliwa baada ya kufikia vigezo vya mashindano.
Hilal alisema kuwa timu hiyo itakuwa chini ya mkuu wa msafara, Amina Mfaume ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TSA na kocha mkuu Samwel Mtupo kutoka klabu ya Mwanza.
“Tunatarajia kupata matokeo mazuri katika mashindano hayo pamoja na ugumu wake. Watanzania zaidi ya milioni 50 wanatarajia kuona mnarejea kishujaa,” alisema Hilal.
Kocha wa timu hiyo, Mtupo alisema kuwa wanajua ushindani katika mashindano hayo na kufanya maandalizi kwa lengo la kufanya vyema.
“Tumejiandaa kwa ajili ya kushindana na tunaamini tutafanya vyema. Naamini waogeleaji waliochaguliwa ambao wana ubora wa hali ya juu, tutajitahidi kuiwakilisha nchi vizuri,” alisema Mtupo.
Nahodha wa timu hiyo, Mohameduwais Abdullatif alisema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya kushinda na siyo vinginevyo.
“Tumefanya maandalizi kwa muda mrefu kwa lengo la kuleta matokeo ambayo Watanzania watayafuraia, ” alisema Abdulatif.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal (kushoto) akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya vijana Mohameduwais Abdullatif.
Waogeleaji wa timu ya Taifa ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi, viongozi wa chama cha kuogelea na wadau mara baada ya kukabidhiwa bendera.
|
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments