Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko, na hisia ambazo hutokea akilini kwa kawaida bila kusudi. Na hii ni katika hatua fulani za usingizi.
Yaweza kuwa alfajiri, asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Lakini kile ambacho kitakuja katika usingizi wako katika onyesho/taswira ndiyo ndoto kamili.
Kimsingi ndoto na uhalisia ni vitu viwili venye tofauti. Ikumbukwe ndoto huleta dhanio, lakini uhalisia ni kile kitu/jambo ambao unaliona kwa nyakati kamili.
Na tukirejea haswa kwa Rich Mavoko na Harmonize kila mmoja ni katika simulizi ya maoni juu yao. Ambapo yote haya ni Harmonize kuonekana ni mwenye kutaka kujiengua kutoka kwenye ‘Genge’ la Wcb.
Wakati huo Rich Mavoko alishajiengua mapema mwaka 2018 kutoka kwenye Genge la Wcb.
Kelele ni nyingi mno, na wapo mahodari wenye kelele haswa. Lakini daima “Mwenye kelele hana neno”
Na hakika kelele nyingi ni za lugha kali za mashabiki lakini wachambuzi pia hofu ni tawala katika hofu kamili juu ya kweli ambayo haihitaji kona.
Kwanza haipaswi kabisa kuweka ufananisho wa Rich Mavoko na Harmonize katika hili la Harmonize.
Ikumbukwe Rich Mavoko alitoka mithili ya mtu awapo ndotoni. Si katika tafakari kuu ya kesho bali usiku wa ndoto pekee.
Harmonize ni katika uhalisia wa kujipanga na uongozi. Lakini egemeo la jamii katika mengi yahusuyo jamii. Lakini kujiongeza kila leo na kuheshimu wengi katika kesho yake.
Rich Mavoko ni katika ndoto ambayo yumwenyewe katika usiku wake. Bila genge la watu nyuma yake lakini hata kujipoteza kwa jamii katika mengi yenye uhitaji wa ushiriki.
Vivyo wenye mfananisho hawapaswi kufananisha wasanii hawa, kwa maana ni wenye tofauti kuu katika uhalisia wao, si mfanano wa ndoto.
Harmonize uwezekano wa kusonga nje wa Wcb upo kwa maana ni mwenye juhudi kamili lakini uhalisia wa nidhamu kuu katika kazi kuanzia ngazi ya mtandao hata nje ya mtandao.
Na uzuri wa Harmonize amejitengeneza yeye na Genge lake la ‘Konde Gang’ kwa upana wa mengi yenye mengi si yale ya ndoto.
Vivyo hakuna uhalisia wa anguko la Harmonize kama ana watu makini katika kesho yake. Bali endelezo lenye ukubwa zaidi.
Pia mkumbuke yakuwa “Mshale kwenda porini haukupotea” (Tafakari..)
By Tizneez
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments