Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli | ZamotoHabari.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Fredrick Cassian Kahimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kahimba umeanza 31 Agosti, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kahimba alikuwa Profesa Mshiriki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.

Prof. Kahimba amechukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini