WAFANYABIASHARA KUJIPATIA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO | ZamotoHabari.



Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WAFANYABIASHARA wengi zaidi kujipatia Leseni za biashara zao kwa njia ya mtandao Oktoba mwanzoni wakiwa huko waliko, huku wakitumia kompyuta na simu zao.

Akizungumza na waandishi wa haari Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andrew Mkapa wilayani Chalinze leo amesema kuwa mafunzo yanayotolewa leo ni kuwajengea uwezo wa watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili kuweza kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao ili kuwasaidia wafanyaiashara kujipatia Leseni hizo kiusahisi.

"Mafunzo haya yanawajengea uwezo wezeshi watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu uanze kutumika kwa majaribio mfumo katika kutoa leseni za biashara kwa njia ya mtandao kwa wafanyabiashara wote nchini".

Amesema kuwa serikali imetoa uamuzi wa kutoa leseni kwa njia ya mtandao kupitia kifungu cha sheria ya biashara namba 25 ya mwaka 1972 zianze kutolewa kwa njia ya mtandao ikiwa Halmashauri sita zimeteuliwa kwaajili ya kutoa mafunzo ya utoaji leseni ya kibiashara kwa njia ya mtandao.

Mfunzo hayo ya utoaji Leseni kwa njia ya mtandao yanatolewa kwenye halmashauri sita nchini ambazo ni Ilala, Chalinze, Mfinga, Mwanza, Bukoba na Karagwe.

Amesema utoaji wa Leseni kwa njia ya mtandao utasaidia kwa urahisi serikali kukusanya mapato, Kupunguza gharama kwa halmashauri zote nchini na kupunguza ghara za kupata Leseni za kibiashara kwa wafanyabiashara.

Licha ya kutoa mafunzo kwa watendaji wa halmashauri zilizoteuliwa hapa nchini changamoto ni uelewa wa wafanyabiashara kwenye mambo ya mtandao.


Ufunguzi wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao utakapozinduliwa hapo mwanzoni mwa Oktoba leseni zitapatikana kupitia websiti ya www.business.go.tz
Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Andrew Mkapa akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chalinze leo wakati wa utoaji mafunzo ya kuwajengea uwezo wa watendaji wa Halmashauri ya Chalinze ili kuweza kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao.
Aliye simama ni Afisa Tehama kutoka Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Samwel Maregeri akitoa mafunzo wa watendaji wa halmshauri ya manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za kibiashara kwa njia ya mtandao. 
Afisa Biashara wilaya ya Chalinze, Zamzam Meja akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipewa mafunzo ya mfumo mpya wa utoaji leseni za biashara kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa Utoaji wa Leseni za kimbiashara kwa njia ya mtandao utasaidia sana katika kutunza muda pamoja na wafanyabiashara hawatapoteza fedha kwaajili ya kufata huduma za utoaji leseni zinapopatikana.
 Afisa Biashara halmashauri ya wilaya ya Chalinze, Samson Moris akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Chalize leo wakati wakipewa mafunzo ya utoaji leseni mpya za kibiashara kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa wataweza kuwahudumia watu wengi zaidi hukohuko waliko na wataweza kupata leseni kwaajili ya kuzitumia katika kufanya biashara zao.
Afisa Tehama wilaya ya Chalinze, Sabuni Joseph akizungumza na waandishi wa habari wilayani Chalinze leo wakati wakipewa mafunzo ya utoaji Leseni Mpy za kibiashara kwa njia ya Mtandao. amesema kuwa amesema kuwa mafunzo hayo ya kutoa Leseni kwa njia ya mtandao yamekuja muda muafaka kwa wafanyabiashara wengi wamekuwa wakipata adha ya kutembea umbali mrefu wakifuata huduma ya kupata Leseni sasa mfumo mpya utawarahisishia kupata Leseni wakiwa hukohuko waliko.
 Watendaji na maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze wakipatiwa mafunzo ya utoaji wa Leseni Mpya za Biashara.

Kulia aliyesimama Afisa Tehama kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Samwel Maregeri akitoa mafunzo wa watendaji wa halmshauri ya manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kutumia mfumo mpya wa utoaji leseni za kibiashara kwa njia ya mtandao.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini