BARABARA YA KIVULE YAANZA KUJENGWA BAADA YA RC MAKONDA KUWASWEKA LUPANGO WAKANDARASI | ZamotoHabari.

Katapila likisawazisha vifusi vilivyomwagwa wakati wa ujenzi wa barabara hiyo katika kona ya Kitunda kwenda Kivule. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA


Daraja lililopo katika barabara hiyo ambalo ni takribani mwaka sasa ujenzi wake haujakamilishwa


Katapila la Kampuni ya Nyanza likiwa kazini katika daraja hilo


Kifusi kimwagwa tayari kwa ujenzi wa barabara hiyo
Kizuizi cha muda kilichichowekwa kurahisisha ujenzi

Na Richard Mwaikenda,Ukonga.

HATIMAYE Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza imeanza ujenzi wa Barabara ya Kitunda-Kivule, Ukonga Dar es Salaam, baada Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutoa amri ya kuwasweka lupango viongozi wa kampuni hiyo.

Makonda alitoa amri hiyo Dar es Salaam Alhamisi, baada ya kampuni hiyo iliyopewa zabuni ya kuchelewa kuanza ujenzi licha ya kulipwa malipo ya awali ya sh. bil. 4.8. Mkataba wa ujenzi umeanza Oktoba Mosi.

Akizungumza na vyombo vya habari, RC Makonda alisema kuwa wakandarasi hao, watakuwa akienda kujenga barabara hiyo wakitokea mahabusu.

Pilikapilika za ujenzi zimeanza ijumaa katika eneo la Kitunda, ambapo yalionekana makatapila yakikwangua sehemu ya barabara hiyo, huku mengine yakisawazisha vifusi vilivyokuwa vinamwagwa na malori.

Kampuni hiyo itajenga kwa kiwango cha lami kipande cha barabara chenye urefu wa km 3.2 kuanzia Kituo cha Polisi Kitunda hadi Mwembeni.

Ubovu wa barabara hiyo ya kutoka Banana, Kitunda hadi Kivule Fremu Kumi, imekuwa ni kero na kilio cha muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo. Ujenzi wa kipande hicho cha barabara unatarajiwa kukamilika Oktoba mwakani.

Kila msimu wa mvua kama huu barabara hiyo uharibika na kuwa na mshimo yanayosababisha daladala nyingi kusita kwenda huko, hali ambayo inawafanya abiria kulipa kiasi kikubwa cha nauli hadi sh.3000 kutoka Banana hadi Flemu Kumi kwa kutumia usafiri wa Bajaji na Bodaboda.

Wakazi wa eneo hilo wameiomba serikali kuwaonea huruma kwa kuhakikisha ujenzi wa kipande hicho kukamilika haraka kabla ya mvua za masika, lakini pia kumalizia kipande kingine cha barabara kutoka Mwmbeni hadi Flemu kumi.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini